Msanii wa tasnia ya filamu nchini Wema Sepetu amezindua filamu yake mpya iitwayo SuperStar huku muigizaji ngulu wa nchini Nigeria Omotola Jalade akiwa mgeni wa busara.
Omotola (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Wema Sepetu
Omotola (kushoto) akibadilishana mawazo na mwenyeji wake Wema Sepetu
Timu ya taifa ya Italy jana iliiondosha katika mashindano ya kombe la Ulaya timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kuchoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya 0-0 katika kipindi cha dakika 120. Picha kwa hisani ya Sky Sports.
Wapenzi wa mabingwa wapya wa ulaya, Chelsea FC ya Uingereza leo walikutata katika fukwe za msasani Beach Club kusherekea ubingwa wa ulaya walioupata msimu huu ulioisha. Wapenzi walisheherekea kwa kufanya michezo mbalimbali pamoja na kupata burudani za muziki kutoka bendi ya Akudo na Muumini Mwijuma.
Mchezaji ambaye usajili wake ulikuwa na utata Kelvin Yondani leo ametambulishwa rasmi katika klabu ya yanga yenye maskani ya ke Jangwani katika kipindi cha mazoezi ya asubuhi klabuni hapo. Yondani aliungana na wachezaji wenzake mara baada ya utambulisho huo.
Kampuni ya IBM ikishirikiana na IBM Tanzania hivi karibuni walizindua teknologia mpya ya PureSytems katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa sherehe wa Hotel ya Hyatt- Kilimanjaro Hotel jijini Daeies-es-Salaam.
Washiriki wakiwa ukumbini Hyatt Kilimanjaro Hotel
Wadau na washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa umakini
Timu ya taifa ya Uingereza jana usiku ilifanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya EURO 2012 baada ya kumfunga mwenyeji Ukrain kwa 1-0 ambapo bao la ushindi la uingereza lilifungwa na mchezaji anayechezea klabu ya Manchester United Wayne Rooney.
Mchezaji Wayne Rooney akipongezwa na mwenzie John Terry mara baada ya mechi kumalizika ambapo Uingereza walishinda 1-0
Katika bunge la leo .. Mheshimiwa John Mnyika mbunge wa jimbo la Ubungo ameamuliwa na naibu spika kutoka nje ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kusema na kukataa kufuta usemi wake kuwa rais Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ni dhaifu katika utendaji wake.. Na ccm na wabunge wake ni wazembe..kwa
utendaji kazi wao..Hii ni kwa mujibu wa taarifa zillizofika hivi punde toka bungeni Dodoma.
Mheshimiwa John Mnyika akichangia mada bungeni
John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania leo mjini
Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu.
Mbunge John Mnyika akisindikizwa na wafanyakazi wa bunge nje ya ukumbi
Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la
Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John
Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni
Taifa juma lililopita lilisikitika kumpoteza Daktari bingwa wa magonjwa ya Kansa katika Hospital ya Ocean Road Dar-es-Salaam ambaye alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa Kansa. Misa ya marehemu ilifanyika katika kanisa katoliki Upanga na baadae mazishi kufanyika kwao Marangu Moshi. Mwanga wa milele umwangazie eeh bwana, apumzike kwa amani amina
Mtoto wa kaka wa marehemu ndg. Frank J. Lyimo akisoma wasifu wa marehemu kanisani
Mkutano mkuu wa kila mwaka ulioandaliwa na benki ya maendeleo Afrika (AFDB) ukishirikisha asasi za kifedha uliofanyika hivi karibuni mkoani Arusha umemalizika kwa mafanikio ikiwa ni pamoja na kuitangaza nchi kimataifa.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wake rais wa Ivory Cost na Rais wa Morrocco