Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Wednesday, June 15, 2011

Dunia imeisha......

WASANII WALA TUNDA LA MTI WA KATI LIVE READERS CLUB

Katia hali isiyo ya kawaida wapigapicha wa gazeti la udaku waliwafumania wasanii hawa wakifanya uchafu wao mchana kweupe! Habari zaidi soma website ya Blog Publihers.

Hapa wasanii wakipeana malavi dave






Hapa wasanii wakipeana mti dawa!






Tuesday, June 14, 2011

Big Brother yadaiwa ni Free Masons.....!

UCHAFU WA WASHIRIKI WA BIG BROTHER WAKIWA MJENGONI

Baadhi ya Wadau wamedai kuwa shindano la Big Brother Amplified ni moja ya uumini wa dini ya Free Masons inayoenea kwa kasi ulimwenguni. Wadau wemethibitisha hilo kutokana na alama ya jicho la kushoto ambalo pia ni moja kati ya alama zinazotumiwa na waumini wa dini hiyo pamoja na matendo ya washiriki wa jumba hilo ikiwa ni pamoja na ulevi wa kupindukia na matendo ya ngono.

Alama ya inayowakilisha Big Brother Amplified.

 
 
 
Mshiriki toka Tanzania akienda kinyume na maadili ya dini zetu kwa kufanya ngono hadharani.

Clinton in Dar....

JK MEETS HILLARY CLINTON AT STATE HOUSE



JK and HC at the State House

Thursday, June 9, 2011

BAJETI 2011/2012 ....!

WABUNGE WAIKACHA BAJETI

KATIKA hali isiyotarajiwa, baadhi ya mawaziri na wabunge hawakuhudhuria Kikao cha Bunge cha jana jioni, wakati wa kusomwa kwa mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/12 yaliyowasilishwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.

Hotuba hiyo ilisomwa kuazia saa 10.00 jioni na kuchukua muda wa saa 2:15. Hii ni bajeti ya kwanza ya Serikali tangu Rais Jakaya Kikwete alipochaguliwa kwa mara ya pili kuongozi nchi, kama ilivyo kwa Bunge la 10 ambalo linapokea na kujadili kwa mara ya kwanza bajeti hiyo chini ya uongozi wa Spika Anne Makinda.

Hata hivyo, kulikuwa na idadi kubwa ya
viti vilivyokuwa wazi wakati Waziri Mkulo alipokuwa akisoma bajeti hiyo na haikufahamika mara moja sababu za baadhi ya mawaziri na wabunge wengi kutohudhuria tukio hilo muhimu la kitaifa.

Jana ilikuwa ni siku ya tatu au kikao cha tatu cha Mkutano wa Nne wa Bunge la 10, ambao ulianza juzi, lakini tofauti na vikao vilivyowahi kufanyika ambavyo huwa na idadi kubwa ya wabunge wakati Serikali ikiwasilisha bajeti yake, kikao hicho kilikuwa na wabunge wachache.

Akizungumza mara baada ya kusomwa kwa bajeti hiyo jana, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema hali hiyo inaweza kusababishwa na baadhi ya wabunge kukata tamaa.

“Inawezekana wanaona bajeti ni yaleyale ya kila siku na wakifikiria Bunge hili ni refu wakadhani hakuna umuhimu wa kuja, jambo ambalo siyo sahihi,” alisema Hamad.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR -Mageuzi), David Kafulila ambaye alisema: “Tatizo ni kwamba wabunge walikata tamaa kabla ya bajeti haijasomwa, wanaona kama hakutakuwa na jipya.”

Hata hivyo, hali ilikuwa ni tofauti kwa wageni ambao walikuwa wengi kiasi cha wahudumu wa Ofisi ya Bunge kulazimika kuongeza idadi ya viti katika baadhi ya sehemu za wageni ambao wengi walikuwa kutoka katika taasisi mbalimbali vikiwamo vyama vya siasa, viongozi wa dini, mabalozi, wakuu wa mashirika ya kimataifa, viongozi wastaafu na wakuu wa vyombo vya dola.

Miongoni mwa waliohudhuria walikuwa ni Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Makatibu
Wakuu wa Wizara, Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Wakuu wa Mikoa, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, Ulaya, vyama vya wafanyakazi, vyombo vya habari
pamoja na taasisi mbalimbali.

Kuwasili eneo la Bunge
Waziri Mkulo aliwasili katika Viwanja vya Bunge saa 9.46 akiwa na mkoba (brifcase) uliokuwa umebadikwa stika yenye nembo ya Serikali katika pande zake mbili na maandishi yaliyosomeka "BAJETI YA SERIKALI 2011/2012."

Mara baada ya kushuka kwenye gari lake, waziri huyo aliunyanyua mkoba juu wake na kuugeuza kila upande, hivyo kutoa fursa kwa wapigapicha wa vyombo
mbalimbali vya habari waliokuwapo kunasa tukio hilo la kihistoria.

Saa 09.48, Mkulo aliingia katika lango kuu la Bunge, lakini hakwenda moja kwa moja ukumbini na badala yake alipumzika katika sehemu ya maalumu
akisubiri kuitwa na Spika.

Spika wa Bunge, Makinda aliingia ukumbini saa 09.58 akiongozwa na mpambe wa Bunge pamoja na makatibu wasaidizi watatu, ambao walikuwa ni wanaume wawili na mwanamke, na baada ya Siwa kuwekwa mahala pake wote walichukua nafasi zao kisha Spika kutoa ruhusa kwa wabunge kuketi.

Wabunge hao walikuwa wamesimama kutii mbiu iliyopigwa saa 09.57 na mpambe wa Bunge, ikiashiria kwamba Spika alikuwa tayari kuingia ukumbini.

Baada ya hatua hiyo, Spika alitoa fursa kwa Katibu kusoma ratiba ya tukio lililokuwa likifuata. Katibu huyo alisema: "Hoja za Serikali, hoja ya Waziri wa Fedha na
Uchumi," baada ya hapo Spika alimwita Waziri Mkulo kufika mbele ya Bunge na kuwasilisha Bajeti ya Serikali.

Mara milango miwili ya lango kuu la kuingia katika ukumbi wa Bunge ilifunguliwa na Waziri Mkulo aliingia ukumbini hapo akiongozwa na mmoja wa askari wa Bunge na kwenda moja kwa moja katika kizimba. Wakati wote huo alikuwa akisindikizwa na makofi ya wabunge.

Wakati Mkulo akitamka neno la kwanza katika hotuba hiyo ambalo ni "Mheshimiwa Spika...." Ilikuwa imetimu saa 10.00 jioni.

Wabunge wakunwa
Wakati Waziri Mkulo akisoma bajeti hiyo, wabunge walikuwa wakipiga makofi mara kwa mara ikiwa ni ishara ya kupongeza vipengele mbalimbali vilivyokuwamo na makofi yaliyochukua muda mrefu zaidi ni wakati Waziri Mkulo alipotangaza hatua za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Miongoni matumizi hayo ni kudhibiti mishahara hewa, kupunguza idadi ya kaunti katika mamlaka za miji na mitaa nchini, kupunguza posho zisizo na tija, kupunguza safari za nje na ukubwa wa misafara ya viongozi na kupunguza semina na warsha ambazo kufanyika kwake kutaendelea kuhitaji kibali cha Waziri Mkuu.

Ilipotimu saa 11.51 Spika Makinda alilazimika kuwatuliza wabunge ambao walionekana kuanzisha mijadala midogo midogo isiyo rasmi baada ya Waziri Mkulo kutangaza ongezeko la faini kwa madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani, kutoka Sh20,000 za sasa hadi Sh50,000. Awali, katika hotuba yake, faini hiyo ilikuwa imependekezwa hadi kufikia Sh300,000.