Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Friday, May 24, 2013

KONGAMANO LA MAAFISA UNUNUZI NA UGAVI LAANZA MOROGORO

Kongamano la pili la maafisa Ununuzi na Ugavi Serikalini limeanza leo mjini Morogoro katika ukumbi wa Hoteli ya Nashera.
Kongamano hilo lililoandaliwa na Idara Sera ya Ununuzi wa Umma chini ya Wizara ya Fedha likiwa na kauli mbiu "Ununuzi Makini kwa Maendeleo ya Taifa" linatazamiwa kuwa la siku mbili kuanzia tarehe 24-25 Mei 2013.

Wajumbe wa Mkutano

Wajumbe wa Sekretarieti

Wajumbe wa Sekretarieti.


Sunday, May 12, 2013

MABALOZI WA UMOJA WA ULAYA WASHEHEREKEA SIKU YAO KWA KUCHEZA MECHI NA WIZARA YA FEDHA

Mabalozi wa nchi za Umoja wa Ulaya EU jana walisheherekea siku yao kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu katika uwanja wa Karume kwa kupambana na timu ya Wizara ya Fedha (Hazina Sports).
Matokeo katika mchezo huo ni kwamba Mabalozi wa EU waliondoka uwanjani kifua mbele kwa ushindi wa mabao 5-2 dhidi Wizara ya fedha

Zawadi ya Ngao kama ishara ya Ushirikiano 
 
Timu ya Wizara ya Fedha
 
 
Timu ya Mabarozi wa Ulaya
 
 
Timu zote mbili kwa pamoja baada ya mchezo.
 

Sunday, May 5, 2013

BOMU LALIPUKA NA KUJERUHI KANISANI ARUSHA

Bomu linalosemekana ni la kurusha limelipuka na kujeruhi watu kadhaa kanisani mkoani Arusha. Vyanzo vya habari vinadai bomu hilo lililipuka wakati wa sherehe za ufunguzi wa kanisa.




Baadhi ya majeruhi wakiugulia maumivu makali mara baada ya mlipuko


b

Friday, May 3, 2013

SODOMAAAA!!! KANGA MOJA WAJA NA STAILI YA KUJIMWAGIA POMBE!

Kikundi cha kucheza michezo ya wakubwa maarufu jijini kama kanga Moja laki si Pesa wamekuja na staili chafu ya kumwagia pombe makalio wakati wa kucheza! Naomba radhi kwa picha hizi ila ndio ukweli wenyewe.












Thursday, May 2, 2013

BONANZA LA MEI MOSI LEADERS CLUB LATIA FORA

Bonanza la Mei Mosi lililoandaliwa na kampuni ya Butterfly Advertising wakishirikiana kipindi cha Sports Extra kinachorushwa na Clouds FM chini ya mtangazaji Shafii Dauda lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club siku ya Mei Mosi lilifana kwa kupendeza.

Tamasha hilo lilizishirikisha timu za mpira wa miguu kutoka makampuni mbali mbali yakiwemo Benk ya CRDB, NMB,Vodacom, FastJet, NSSF, Tanesco, Umoja water, NHC, Clouds FM na DHL.
Katika mshindano hayo Tanesco waliibuka mabingwa baada ya kuilaza FastJet katika mchezo wa fainali kwa bao 1-0. Habari zaidi katika picha.






Bendi ya Skylight ikitumbuiza mara baada ya michezo kumalizika

SIKUKUU YA MEI MOSI YAFANA

Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ilisheherekewa kwa namna yake ulimwenguni huku ha kwetu tanzania ikipambwa na maandamano ya wafanyakazi katka viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar-es-Salaam. Katika sherehe za mwaka huu, rais wa Jamhuri ya Tanzania Dr. Mrisho Jakaya Kikwetealihaidi serikali kupunguza kodi ya mshahara kwa wafanyakazi. Habari zaidi katika picha.


Wednesday, May 1, 2013

BAHATI YAITOA MADRID UEFA

Timu ya Real Madrid ya Hispania usiku wa leo wamelala vibaya baada ya kujikuta wanaondoshwa katika nusu fainali ya kombe la UEFA na klab ya Dortmund ya Ujerumani kwa idada ya mabao 4-2 baada ya kucheza mchezo wa marudiano.