Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Tuesday, March 26, 2013

KONA YA MAPENZI...

USAFI KATIKA MAPENZI

KILA mmoja wetu anafahamu nini maana ya usafi, lakini baadhi ya watu wamekuwa hawatilii maanani, hawana habari, hawajali pia wapo wengine hawajui kabisa waanzie wapi kuwa wasafi. Na ile kauli ya kwamba mapenzi hayana chafu yamepitwa na wakati kutoka na kuongezeka kwa magonjwa mbali mbali siku hizi.

Mapenzi yanahusisha mambo na maungo mbalimbali kama vile miguu (legs), miguu ya kukanyagia (feet) na kucha zake, mikono, viganja ikiwa ni pamoja na kucha zake,macho, pua, midomo ya nje (lips), kinywa, nyayo, makalio, alafu ndio zinafuata sehemu nyeti.
Maungo hayo yote yanamaana na umuhimu wake katika swala zima la mapenzi hasa yakitumiwa ipasavyo na yakiwekwa katika hali ya usafi, vinginevyo utampoteza mpenzi wako au kuharibu uhusiano wenu mzuri mlionao.
Usafi ninaouzungumzia hapa sio ule wa kuoga na kupaka Manukato (perfum)/Lotion/mafuta, kufua/kunyoosha nguo pekee bali ni usafi ule wa ndani ambao baadhi ya wanawake hufundishwa tangu wakiwa na umri mdogo.
Hali kadhalika wanaume pia hufundishwa jinsi ya kujisafi baadhi ya maeneo ya miili yao, lakini inasikitisha kuwa wanaume wengi hawajali kabisa usafi uwe ni ule wa kawaida au ule wa kunako nyeti.
Wapo baadhi ya wanume na wanawake ambao hupenda sana kulambwa lambwa katika maeneo Fulani ya miili yao wakidai kuwa ndio inayowaongezea nyege, lakini cha kusikitisha ni kuwa watu hawa hawajali/hawatunzi maeneo hayo na badala yake kutegemea mwanamke amshughulikie.
Leo nitazungumzia utunzaji wa kinywa na kunako majaaliwa nitaelezea umuhimu wa kila kiungo nilichokitaja hapo awali na utunzaji wake.
*Sugua meno yako kila siku asubuhi na jioni, ikiwezekana kila baada ya kula chakula. Anza kwa kusugua meno pande zote juu, chini, katikati na pembeni, hakikisha kila pande unatumia dakika kumi.
*Safisha mswaki wako na usugue ulimi wako sehemu ya katikati na pembeni rudia mpaka ukitema mate yasiwe na mrendamrenda, kisha suuza na maji ya vuguvugu.
*Ikiwa “unaasili” ya kuwa na nyuzinyuzi katika kinywa yaani ukiongea/kucheka/ kupiga miayo n.k kunatokea mate yaliyoungana mithili ya uzi, hali hiyo hakika hutia kichefuchefu.
Unachotakiwa kufanya kila baada ya kula ni kutafuna kipande cha limau/ndimu/mbilimbi/mdalasini ambayo itasaidia kukata mate au tafuna bazoka zenye MINT (Bongo zipo na zinauzwa Tsh.2,000 kwa paketi) ambazo hazijaongezewa sukari ili kuepusha harufu mbaya ya kinywa na meno yako yasioze.
Usikukose kutembelea hapa ili jue jinsi yakujiswafi maeneo mengine kwa njia ya asili ambayo si ghali kwa watanzania wengi na ile ya kileo ambayo tunawaachia wenye kuweza.
Siku njema. (Makala na Oooooh itie Yote)