Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Saturday, April 7, 2012

Breaking News...... Steven Kanumba afariki Dunia!

MASKINI KANUMBA...MAJONZI NCHI NZIMA !

Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican. Chazo kinasema Kanumba alitoka kuoga na kumkuta Lulu ambaye inasemekana ni wapenzi akiongea na simu ndipo hapo ugomvi ulipoanzia mpaka kanumba kujikuta akidondokea kisogo na kutokwa na damu nyingi. 
 
Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi, mdogo wake kanumba athibitisha uwepo wa lulu wakati Kanumba akipatwa na matatizo yaliyosababisha kifo chake, anasema wawilihao walikuwa na mabishano makubwa kabla ya Lulu hajatoka ndani kumuita na kumwambia kwamba Kanumba amedondoka na anatokwa na mapovu mdomoni.



HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
 
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
 
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
 
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
 
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
 
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
 
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
 
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

No comments:

Post a Comment