MSANII WA BONGO FLEVA MR. EBBO AFARIKI DUNIA.
Habari zilizotufikia hivi karibuni zinasema yule msanii wa Muziki wa bongo Fleva anayetumia rafudhi ya Lugha ya kimasai katika kuimba mashairi yake maarufu kama Mr. Ebbo (Abel Motika) amefariki dunia leo alfajili jijini Arusha.
Marehemu Mr. Ebbo
Msanii Dogo Dito akiomba dua ya kumwombea Mr. Ebbo live katika studio za Clouds Tv. Picha kwa hisani ya Clouds Tv.
Habari zinasema marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu kabla ya umauti kumkuta. Familia nzima ya Blog hii inawapa pole ndugu na jamaa kwa msiba huu! Mungu ailaze pema roho ya marehemu peponi amina.
No comments:
Post a Comment