BANK YA KCB YATOA MSAADA WA VISIMA
Friday, December 30, 2011
Uhaba wa Maji...
Harusi.....
MUIGIZAJI KUTOKA NIGERIA "AKI" AACHANA NA UKAPERA!
Busu zito la bibi harusi Mwaaaa!
Bibi harusi akila kiapo cha ndoa
Bibi na bwana harusi baada ya kufunga ndoa
Bibi harusi akiketi ili akumbatiwe vizuri!
Best man Ukwa na P-Squre wakipiga picha na Maharusi!
Best Man Ukwa na bwana harusi Aki
Maharusi wakifungua mziki!
Gari lililowabeba bwana na Bibi harusi
(Picha kwa hisani ya kanumba the great)
(Picha kwa hisani ya kanumba the great)
Wednesday, December 28, 2011
Masaada!
VODACOM TANZANIA YAHAMASISHA KUCHANGIA WAHANGA WA MAFURIKO
Ndugu zetu waliopatwa na janga la mafuriko bado wanahitaji misaada yetu Watanzania tafdhal endelea kuchangia kwa Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.
Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa
*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7: Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.
Sunday, December 25, 2011
Merry X-Mass!
SIKUKUU NJEMA WADAU
Menejimenti ya Blog nzima ya Njia ya Kanani inapenda kuwatakia sikukuu njema za X-Mass na mwaka mpya wa 2011 wadau wote wanaotembelea blog hii na wale ambao hawajawahi na kuwaahidi kuboresha habari ma matukio yanayojili. Mungu awabariki nyote!
Friday, December 23, 2011
Breaking News...!
BASI LA NGORIKA YAPATA AJALI
Basi la Ngorika limepata ajali leo mida ya saa 4 asubuhi maeneo ya Mkata likielekea Moshi kutoka Da-es-salaam na kupinduka pembeni ya barabara. Habari zinasema hakuna abilia aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Athari za Mafuriko ya Dar.....!
MAISHA YAANZA UPYA BAADA YA MAFURIKO
Wakazi wa jiji la Dar-es-Saalaam wameaanza maisha yao upya baada ya kunusurika kwenye mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali iliyonyesha usiku wa kuamkia jana na juzi jijini.
Wakazi wa jangwani wakifanya ukarabati ili waendelee na maisha
Moja ya kambi za waathirika.
Mawazo kibarazani.
Nguo zikiwa zimeanikwa katika kambi ya waathirika wa mafuriko katika shule ya msingi mchikichini.
Maisha kambini.
Huruma, Familia iliopoteza makazi wakiwa shuleni
Wednesday, December 21, 2011
Mafuriko dar.....!
JIJI LA DAR-ES-SALAAM LAKUMBWA NA MAFURIKO MAKUBWA
Pata habari katika picha;
Nyatare Hall Tabata kama lilivyokutwa leo
Hali inavyoonekana katika Uwanja wa mazoezi wa club ya Yanga Jangwani
Magali yakipita kibarazani Millenium Tower Kijitonyama
Hata mjini mambo si shwari!
Kina mama wakijiokoa na watoto
Hata mbezi napo mambo hayakuwa shwari!
Monday, December 19, 2011
Hekaheka za si hasaaa....
KAFULILA WA NCCR MAGEUZI AVULIWA UANACHAMA
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
Baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya NCCR-Mageuzi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, na wenzake watatu, chama hicho kimewapa siku 14 za kukata rufaa kwenye Mkutano Mkuu kupinga uamuzi huo dhidi yao, huku kikimpa Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali, karipio kali kutokana na kujihusisha na mgogoro katika chama.
Futiboli......
BARCELONA ARE CROWNED WORD CLUB CHAMPIONS
Neymar said Barcelona are "impossible" to defeat after Santos were demolished 4-0 in the Club World Cup final.
Two goals from Lionel Messi either side of strikes from Xavi and Cesc Fabregas provided a convincing victory for the European champions as Neymar and co were unable to make their mark.
"It's impossible to stop Barcelona, but we are the second-best team in the world and for us that is a great reward," Neymar said.
Santos coach Muricy Ramalho offered a similar assessment of a Barcelona side he deems "invincible".
"Barcelona are the greatest team in the world," he said. "No team can live with them. They're unbeatable at the moment. Losing 4-0 to them is no disgrace."
Barcelona didn't have any problem with Santos FC in the Club World Cup final, easily winning 4-0.
Friday, December 16, 2011
Ratiba ya UEFA Champions League.........
Breaking News!!!!!!!!!!!
WASHIKA BUNDUKI WA LONDON WAANGUKIA MDOMONI WA ROSSINELI. (ARSERNALvs AC MILAN)
Timu ya Arsenal ya Uingereza leo mchana imejikuta ikipangwa kucheza na timu kali ya AC Milan ya Italia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya kuingia robo fainali ya Kombe la klabu bingwa barani Ulaya maarufu kama UEFA Champion League. Mechi hizo zitachezwa kati ya Feb 14-15 na marudio yatakuwa Feb 21-22.
Mpanga ratiba wa chama cha soka Ulaya (UEFA) akionesha kikaratasi chenye jina na Arsenal
Ratiba kamili ya roundi ya kumi na sita bora mtoano ni kama ifuatavyo:
First games to be played on Feb 14-15, 21-22
Lyon | v | APOEL Nicosia |
Napoli | v | Chelsea |
AC Milan | v | Arsenal |
FC Basel | v | Bayern Munich |
Bayer Leverkusen | v | Barcelona |
CSKA Moscow | v | Real Madrid |
Zenit St Peterburg | v | Benfica |
Marseille | v | Inter Milan |
...Sakata la Posho za waheshimiwa na Ushoga.....
KADINALI PENGO AUNGURUMA.
- AONYA BILA KATIBA MPYA UCHAGUZI MKUU 2015 UTAKUMBWA NA GHASIA,
- AITA USHOGA NI WENDAWAZIMU.
- AWAAMBIA WABUNGE POSHO SIO WALICHOTUMWA.
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amezungumzia mambo kadhaa ya kitaifa akisema, ongezeko la posho kwa viongozi wa umma ni ubinafsi na kuonya kama Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 utafanyika bila ya kuwako kwa Katiba Mpya, utagubikwa na ghasia.Pengo alitoa angalizo hilo jijini Dares Salaam jana alipokuwa akitoa ujumbe kwa taifa kuhusu Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, Sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Kuhusu posho, Kadinali Pengo alisema viongozi wa Serikali na umma wakiwamo wabunge, wanapaswa kuacha ubinafsi na badala yake wafanye kazi kwa kuwafikiria zaidi wananchi kuliko maslahi binafsi.
“Sisi Wakristu tunaamani kuwa, Kristu licha ya kuwa alitumwa na Mungu Baba kuja kutukomboa wanadamu alifanyika mwili na kuzaliwa katika hali ya umaskini na ufukara ili atukomboe. Viongozi wa Serikali, dini na watumishi wa umma, inatupaswa kuiga mfano huo,”alisema Pengo.
Aliongeza, “Nasisitiza hili kwa viongozi sababu hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya wabunge na wananchi ambao wamejiongeza posho kwa madai maisha kuwa magumu. Viongozi hatupaswi kufikiria marupurupu yetu na maslahi yetu kwanza kabla ya kuwafikiria wananchi tunaowaongoza.”
“Sisi Wakristu tunaamani kuwa, Kristu licha ya kuwa alitumwa na Mungu Baba kuja kutukomboa wanadamu alifanyika mwili na kuzaliwa katika hali ya umaskini na ufukara ili atukomboe. Viongozi wa Serikali, dini na watumishi wa umma, inatupaswa kuiga mfano huo,”alisema Pengo.
Aliongeza, “Nasisitiza hili kwa viongozi sababu hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya wabunge na wananchi ambao wamejiongeza posho kwa madai maisha kuwa magumu. Viongozi hatupaswi kufikiria marupurupu yetu na maslahi yetu kwanza kabla ya kuwafikiria wananchi tunaowaongoza.”
Alipoulizwa kuhusu suala la mataifa makubwa ya Uingereza na Marekeni kutaka mataifa yanayowapa misaada kuwatambua watu wanaojihusisha na ushoga, Kadinali Pengo alijibu kwa kifupi “Ushoga ni wendawazimu”.
Alisema Mungu alipoumba watu; mwanamke na mwanaume na kuwapa hisia, alitaka watu wazaliane na kuujaza ulimwengu. Akahoji “Huyo mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke wanakutana ili iwe nini?”
Pengo alisema wanaoshiriki ushoga wanamkosea Mungu na kusisitiza, kamwe hakutakuwa na furaha kwa mtu anayekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Alisema Mungu alipoumba watu; mwanamke na mwanaume na kuwapa hisia, alitaka watu wazaliane na kuujaza ulimwengu. Akahoji “Huyo mwanaume kwa mwanaume au mwanamke kwa mwanamke wanakutana ili iwe nini?”
Pengo alisema wanaoshiriki ushoga wanamkosea Mungu na kusisitiza, kamwe hakutakuwa na furaha kwa mtu anayekwenda kinyume na mapenzi ya Mungu.
Thursday, December 15, 2011
Wanawake....
KONGAMANO LA MWANAMKE WA KITOFAUTI KUFANYIKA DAR-ES-SALAAM DECEMBER 17
Naibu Mkurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Jacqueline Maleko, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu kongamano la mwanamke wa kitofauti, litakalofanyika Dar es Salaam, Desemba 17, mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya wanawake Tanzania Bi Margaret Chacha.
Matokeo ya Darasa la saba.....
WALIOFAULU WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 90.1
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philipo Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba, Mwaka 2011. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw.Selestine Gesimba. (Majira)
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo ya watahiniwa 9,736 waliofanya mtihani wa kumaliza.
darasa la saba mwaka huu baada ya kubainika kufanya udanganyifu. Pia wanafunzi 567,567 kati ya 983,545 waliofanya mtihani huo ambapo wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90.1 wamechaguliwakuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw.Philipo Mulugo, alisema.
darasa la saba mwaka huu baada ya kubainika kufanya udanganyifu. Pia wanafunzi 567,567 kati ya 983,545 waliofanya mtihani huo ambapo wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90.1 wamechaguliwakuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw.Philipo Mulugo, alisema.
Alisema kati ya wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu wapo wavulana 4,943 na wasichana 4,793. Alitaja aina za udangayifu waliofanya kuwa ni pamoja na watahiniwa 94 kukutwa na karatasi na rula zenye majibu pamoja na viatu aina ya ‘yeboyebo’, zikiwa na majibu ya mtihani. Alisema wanafunzi hao walikamatwa katika Halmashauri za Bukoba mkoani Kagera, Muheza mkoani Tanga, Maswa mkoani Shinyanga, Sumbawanga mkoani Rukwa, Mtwara, Lindi na Tarime mkoani Mara.
Akizungumzia malalamiko ya kuwepo kwa wanafunzi wanaofaulu mtihani huo bila kujua kusoma na kuandika, Bw.Mulugo alisema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, watafanya mtihani wa kujipima kabla ya kuanza masomo. “Mwanafunzi ambaye itabainika amejiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi husika, Mwalimu Mkuu wa shule aliyotokea mwanafunzi na msimamizi wa mtihani watachukuliwa hatua za kinidhamu," alisema.
Michano live....
WASANII WA BONGO MOVI KUNAFUKUTA....
Wasanii wa Bongo movie wakichanana live katika kipindi cha Bongo Movie kinachorushwa na Clouds TV katika segment ya take one. (Kwa hisani ya kajunason Blog)
Ndoto alizokuwa nazo zimefutika.........! Duh! Kama tungekewa tunajua ya mbeleni basi tungekuwa tunakaa kimnya tu! Diamond a.k.a Sukari ya mabinti sijui alitoa wapi hii a.k.a. Pata video ya mwanadada Wema akifunguka hapo kabla!
Hii ilkuwa kwenye show Morogoro Fiesta!
Wema akivalishwa pete!
Wema akivalishwa pete!
Wednesday, December 14, 2011
Dunia imeisha....!
MAMA MTU MZIMA AMWAGA RADHI KWEUPE PEE!NA KUMFANDHAISHA BABU
Mama mmoja mtu mzima alifumaniwa uswahilini akimwaga radhi mbele ya umati wa watu uliojaa watoto na watu wazima baada ya kupandisha mzuka wa taarabu na kujikuta anazungusha nyonga kiasi cha kufikia kuvua nguo. Katika kituko hicho babu mmoja wa makamo alionekana kushabikia kiasi cha kumfanya apate mfadhaiko na kujichafua!
Mambo yalianza hivi baada ya kulisikia taarab....juma! juma! wewe...!
Mara, Babu akaanza tamaa...........
Ooooh! Babu akaona isiwe tabu......
Babu akaendelea na kuamua kujimilikisha kwa kukataza wengine kugusa.....!
(Picha nyingine zimeondolewa kutokana na kuwa kinyume na maadili)
Wahisani....
MAGAVANA WA ADB KUKUTANA ARUSHA
Mkutano Mkuu wa Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), unatarajia kufanyika jijini Arusha kuanzia Mei 30 hadi Juni Mosi, mwakani. Hayo yalisemwa jana na Mwakilishi Mkazi wa AFDB, Dk. Tonia Kandiero, wakati akizungumza na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya kwenda kujitambulisha.
Rais Kikwete akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Tonia Kandiero, aliyemtembelea jana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana ilieleza kuwa Dk. Kandiero, alisema kuwa pamoja na mambo mengine, amekwenda Ikulu kumueleza rasmi Rais Kikwete kuhusu mkutano huo wa magavana hao ambao hata hivyo hakufafanua yatakayojadiliwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, AfDB ni moja ya wahisani wakubwa wa Tanzania kwa kutoa misaada kwenye miradi ya maendeleo na hasa sekta za barabara, kilimo, maji na nishati. (Chanzo: Nipashe)
Tuesday, December 13, 2011
Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru....
WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo na Naibu wake Dkt Shaaban Mwinjaka, wakimpokea Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda kutembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika siku ya mwisho ya Maonesho ya miaka 50 ya Uhuru ya Uhuru Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo akimpa maelezo Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda juu ya hatua mbali mbali za mafanikio zilizofikiwa na Wizara yake kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru
Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Eline Sikazwe akimueleza Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika Idara yake.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini yake mara baada ya kufungwa kwa maonesho ya miaka 50 ya katika Viwanja vya Mwl J.K.Nyerere. Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara limekuwa kivutio kikubwa kwa wageni kutokana na maandalizi mazuri na bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na Viwanda vya Tanzania. Picha kwa hisani ya Fullshangwe Blog.
Sakata la Posho za wabunge....
POSHO ZA WABUNGE ZASIMAMISHWA ZIKISUBILI MAAMUZI YA JK
Ongezeko jipya la posho za waheshimiwa wabunge hazitoendelewa kugawiwa mpaka litakapotoka tamko rasmi kutoka kwa mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na ongezeko hilo.
Wiki iliyopita, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda alitangaza mjini Dar-es-Salaam kuwa posho za wabunge sasa zimeongezwa kwa asilimia 185 hadi kufikia shilingi 200,000 kwa siku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)