Jana usiku spain walitangazwa kuwa mabingwa wa EURO 2012 baada ya kuikung'uta Italy kwa mabao 4-1 yaliyofungwa na David Silva, Jordi Alba, Fernando Toress na Juan Mata.
Msanii wa tasnia ya filamu nchini Wema Sepetu amezindua filamu yake mpya iitwayo SuperStar huku muigizaji ngulu wa nchini Nigeria Omotola Jalade akiwa mgeni wa busara.
Omotola (kushoto), akiwa na mwenyeji wake Wema Sepetu
Omotola (kushoto) akibadilishana mawazo na mwenyeji wake Wema Sepetu
Timu ya taifa ya Italy jana iliiondosha katika mashindano ya kombe la Ulaya timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kuchoshana nguvu kwa kutoka suluhu ya 0-0 katika kipindi cha dakika 120. Picha kwa hisani ya Sky Sports.
Wapenzi wa mabingwa wapya wa ulaya, Chelsea FC ya Uingereza leo walikutata katika fukwe za msasani Beach Club kusherekea ubingwa wa ulaya walioupata msimu huu ulioisha. Wapenzi walisheherekea kwa kufanya michezo mbalimbali pamoja na kupata burudani za muziki kutoka bendi ya Akudo na Muumini Mwijuma.
Mchezaji ambaye usajili wake ulikuwa na utata Kelvin Yondani leo ametambulishwa rasmi katika klabu ya yanga yenye maskani ya ke Jangwani katika kipindi cha mazoezi ya asubuhi klabuni hapo. Yondani aliungana na wachezaji wenzake mara baada ya utambulisho huo.
Kampuni ya IBM ikishirikiana na IBM Tanzania hivi karibuni walizindua teknologia mpya ya PureSytems katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa sherehe wa Hotel ya Hyatt- Kilimanjaro Hotel jijini Daeies-es-Salaam.
Washiriki wakiwa ukumbini Hyatt Kilimanjaro Hotel
Wadau na washiriki mbalimbali wakifuatilia kwa umakini
Timu ya taifa ya Uingereza jana usiku ilifanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya EURO 2012 baada ya kumfunga mwenyeji Ukrain kwa 1-0 ambapo bao la ushindi la uingereza lilifungwa na mchezaji anayechezea klabu ya Manchester United Wayne Rooney.
Mchezaji Wayne Rooney akipongezwa na mwenzie John Terry mara baada ya mechi kumalizika ambapo Uingereza walishinda 1-0