Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.
Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.
Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.
wanafunzi wa Chuo cha IFM wakiwa nje ya Wizara ya mambo ya ndani
Kiongozi wa wanafunzi akimjuza kamanda Kova
Kama kawaida yao walikuwepo!
Maandamano kuelekea ferry...
Hatimaye wakiwa wanaimba nyimbo ndani ya Panton...
No comments:
Post a Comment