Mheshimiwa Rais akikagua moja ya makanisa yaliyochomwa moto
Sio ujenzi wa msikiti, hapana ni waumini wakiokota mawe tayari kwa mashambulizi
Chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la
Mbagala kizuiani Wilaya ya Temeke jijini Dar-es-Salaam imeelezwa
kusababishwa na mama mzazi wa Emmanuel Josephat (14) anayetuhumiwa
kukojolea Qur'an kutoa lugha ya kejeli na kashfa dhidi yatukio hilo.
Mama huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja imeelezwa kwamba alikejeli tukio hilo na kugoma kumsikiliza mzazi mwenzie ambaye mwanae alinyang'anywa Qur'an na kusema kwamba yeye alidhani ni jambo la kutisha kama kuua kumbe suala lenyewe ni dogo na lisilo na maana,"nilidhani mwanangu kaua kumbe jambo lenyewe ni hili dogo" alisema mama huyo.
Imeelezwa kwamba mama huyo alikuwa tatizo hadi hapo baba mzazi wa mtoto alinyang'anywa Qur'an Hamis Saluum Mbonde kufika nyumbani kwa mama huyo kutaka kufanya mazungumzo katika kupata ufumbuzi.
Kisiwa limebainishwa kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano Oktoba 10 saa 12 jioni, ambapo vijana hao walianza kubishana juu ya kitabu hicho ndipo Emmanuel aliamua kukikojolea.
Mabishano hayo yalianza baada ya Emmanuel kumuuliza Zakaria maana ya kitabu hicho na alipojibiwa alimweleza kwamba anaweza akafanya chochote na asipatwe lolote.
Baada ya mabishano hayo, walifika katika uwanja wa mpira na kisha Zakaria akatoa mpira wake na kuwapa vijana waliokuwa uwanjani hapo na kuanza kucheza.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa baada ya Zakaria kuweka kitabu chake mahala alipoona panafaa aliingia uwanjani na kuanza kucheza mpira na wenzake na mara Emmanuel akaonekana akifungua zipu na kukojolea kitabu hicho.

No comments:
Post a Comment