Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Tuesday, October 23, 2012

ALIYEKUA KATIBU CHADEMA ARUSHA AACHIWA HURU

 
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha, imemwachia huru aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Arusha mjini Gervas Mgonja pamoja na watuhumiwa wengine wawili, baada ya mahakama hiyo kuthibitisha kutokuwa na kesi ya kujibu iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.

Akitoa maamuzi madogo (rulling) mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa mahakama kuu, Judith Kamala kwa kushirikiana na Mwendesha mashtaka wa Serikali, Haruna Matagane alisema kuwa, mahakama imeamua kumwachia huru mshitakiwa huyo na wenzake wawili baada ya kubaini kuwa hawana kesi ya kujibu katika shitaka la kula njama na kutenda kosa lililokuwa likiwakabili.

Mgonja alishtakiwa na wenzake wawili – aliyekuwa katibu wa vijana wa CHADEMA wilaya ya Arusha, Arnold Kamnde na Frank Njau aliyekuwa Katibu wa Vijana kata ya Ngarenaro CHADEMA.

     Baada ya kupitia upande wa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao walileta mashaidi sita, Hakimu Kamala alisema washtakiwa hao watatu kwa pamoja walikuwa wakishitakiwa na wenzao wengine watatu (jumla sita) kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo upelelezi ulipokamilika ulibaini kuwa washitakiwa watatu akiwemo Mgonja walifungliwa shitaka hilo la unyang’anyi wa kutumia silaha kimakosa na hivyo mahakama kuwaondoa katika shitaka hilo na kubakia na washatakiwa watatu ambao wanaendelea na kesi hiyo.

Washitakiwa waliobakia na kesi hiyo ni Frank Ismail, Philemon Inyasi na Charles George.

Awali, Mgoja na wenzake walikaa ndani kwa siku 120 tangu walipofunguliwa shitaka hilo Agosti 20 mwaka jana hadi upelelezi ulipokamilika Januari 15 mwaka huu na kuwaondoa katika kesi hiyo na kusomewa shitaka jipya la kula njama ya kutenda kosa, ndipo walipopewa dhamana.

Kesi hiyo mpya ilianza kusikilizwa Januari 15 mwaka huu na kesi ilirindima kwa kipindi cha miezi kumi hadi maamuzi.
 


No comments:

Post a Comment