Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Wednesday, October 31, 2012

ZIARA YA RAIS MKOANI KILIMANJARO YASABABISHA FOLENI KAMA ZA DAR

Ziara ya Mh. Dr. Mrisho Jakaya Kikwete rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mkoani kilimanjaro imesababisha adha kubwa ya foleni baada ya askari wa barabarani kusimamisha magari kwa muda wa takribani lisaa limoja na nusu. Hii ilisababisha kuwepo kwa msongamano wa foleni kwa magari yaliyokuwa yakitokea Dar-es-Salaam.


Wednesday, October 24, 2012

GARI DOGO LAWAKA MOTO LEO ASUBUHI

Gari ndogo aina ya Nissan Pick-up leo katika barabara ya Kilwa round about ya Mivinjeni limeteketea kwa moto uliosababishwa na hitirafu ya umeme katika gari hilo. Dereva alisalimika na hakuna kilichookolewa.




SUMATRA NA WADAU KUJADI NAULI YA TRENI LEO

SUMATRA leo wamewaalika wadau wa usafili jijini kwenda kujadili nauli mpya ya usafiri wa treni ya mjini itakayoanzia stesheni posta hadi ubungo maziwa.

Majadiliano hayo kati ya wadau na SUMATRA yatakuwa ni juu ya kujadili bei elekezi iliyototewa na kampuni ya reli (TRA).

Tuesday, October 23, 2012

ALIYEKUA KATIBU CHADEMA ARUSHA AACHIWA HURU

 
MAHAKAMA kuu kanda ya Arusha, imemwachia huru aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Arusha mjini Gervas Mgonja pamoja na watuhumiwa wengine wawili, baada ya mahakama hiyo kuthibitisha kutokuwa na kesi ya kujibu iliyokuwa ikiwakabili mahakamani hapo.

Akitoa maamuzi madogo (rulling) mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa mahakama kuu, Judith Kamala kwa kushirikiana na Mwendesha mashtaka wa Serikali, Haruna Matagane alisema kuwa, mahakama imeamua kumwachia huru mshitakiwa huyo na wenzake wawili baada ya kubaini kuwa hawana kesi ya kujibu katika shitaka la kula njama na kutenda kosa lililokuwa likiwakabili.

Mgonja alishtakiwa na wenzake wawili – aliyekuwa katibu wa vijana wa CHADEMA wilaya ya Arusha, Arnold Kamnde na Frank Njau aliyekuwa Katibu wa Vijana kata ya Ngarenaro CHADEMA.

     Baada ya kupitia upande wa ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao walileta mashaidi sita, Hakimu Kamala alisema washtakiwa hao watatu kwa pamoja walikuwa wakishitakiwa na wenzao wengine watatu (jumla sita) kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo upelelezi ulipokamilika ulibaini kuwa washitakiwa watatu akiwemo Mgonja walifungliwa shitaka hilo la unyang’anyi wa kutumia silaha kimakosa na hivyo mahakama kuwaondoa katika shitaka hilo na kubakia na washatakiwa watatu ambao wanaendelea na kesi hiyo.

Washitakiwa waliobakia na kesi hiyo ni Frank Ismail, Philemon Inyasi na Charles George.

Awali, Mgoja na wenzake walikaa ndani kwa siku 120 tangu walipofunguliwa shitaka hilo Agosti 20 mwaka jana hadi upelelezi ulipokamilika Januari 15 mwaka huu na kuwaondoa katika kesi hiyo na kusomewa shitaka jipya la kula njama ya kutenda kosa, ndipo walipopewa dhamana.

Kesi hiyo mpya ilianza kusikilizwa Januari 15 mwaka huu na kesi ilirindima kwa kipindi cha miezi kumi hadi maamuzi.
 


KUTANA NA MBWA ALIYEFUNDISHWA UBAKAJI



Tuesday, October 16, 2012

VURUGU ZA MBAGALA NANI ALAUMIWE?

Mheshimiwa Rais akikagua moja ya makanisa yaliyochomwa moto




Sio ujenzi wa msikiti, hapana ni waumini wakiokota mawe tayari kwa mashambulizi
 
Chanzo cha vurugu zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Mbagala kizuiani Wilaya ya Temeke jijini Dar-es-Salaam imeelezwa kusababishwa na mama mzazi wa Emmanuel Josephat (14) anayetuhumiwa kukojolea Qur'an kutoa lugha ya kejeli na kashfa dhidi yatukio hilo.
Mama huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja imeelezwa kwamba alikejeli tukio hilo na kugoma kumsikiliza mzazi mwenzie ambaye mwanae alinyang'anywa Qur'an na kusema kwamba yeye alidhani ni jambo la kutisha kama kuua kumbe suala lenyewe ni dogo na lisilo na maana,"nilidhani mwanangu kaua kumbe jambo lenyewe ni hili dogo" alisema mama huyo.

Imeelezwa kwamba mama huyo alikuwa tatizo hadi hapo baba mzazi wa mtoto alinyang'anywa Qur'an Hamis Saluum Mbonde kufika nyumbani kwa mama huyo kutaka kufanya mazungumzo katika kupata ufumbuzi.
Kisiwa limebainishwa kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano Oktoba 10 saa 12 jioni, ambapo vijana hao walianza kubishana juu ya kitabu hicho ndipo Emmanuel aliamua kukikojolea.

Mabishano hayo yalianza baada ya Emmanuel kumuuliza Zakaria maana ya kitabu hicho na alipojibiwa alimweleza kwamba anaweza akafanya chochote na asipatwe lolote.
Baada ya mabishano hayo, walifika katika uwanja wa mpira na kisha Zakaria akatoa mpira wake na kuwapa vijana waliokuwa uwanjani hapo na kuanza kucheza.
Taarifa ziliendelea kusema kuwa baada ya Zakaria kuweka kitabu chake mahala alipoona panafaa aliingia uwanjani na kuanza kucheza mpira na wenzake na mara Emmanuel akaonekana akifungua zipu na kukojolea kitabu hicho.

Monday, October 8, 2012

MTAALAM KUTEGA WEZI WA WAUME NA WAKE ZA WATU AINGIA DAR

Yule mtaalam mwenye dawa ya kutega wanaume na wanawake wakware waliozoea kuiba wake na waume za watu na kufanya wang'ang'aniane wakati wakifanya uchafu wao inasemekana ameingia mjini toka nchini Uganda ambapo alikuwa akifanya shughuri zake huko.

Hii ni moja ya kazi zake

YALIYOJILI FIESTA 2012

Tamasha la Fiesta 2012 lililoandaliwa na Clouds FM mwaka huu lilikuwa na kufana na mafanikio kama picha chini zinavyojionesha.
Picha kwa hisani ya Full Shangwe Blog.

Ross akichengua mashabiki ndani ya fiesta

Lina akiwa katika jukwaa la fiesta

 Michael Jackson wa Bongo





 Umati ulifurika

 Pah one!

 Bahati nasibu ya Serengeti ikichezeshwa

Polisi wa Bongo kama kawaida yao

Friday, October 5, 2012

EUROPA LEAGUE

Europa League - Results:
Newcastle Utd 3 - 0 Bordeaux,
Liverpool 2 - 3 Udinese,
Atletico Madrid 1 - 0 Viktoria Plzen,
PSV Eindhoven 3 - 0 Napoli,
Monchengladbach 2 - 4 Fenerbahce,
Marseille 5 - 1 AEL Limassol

Thursday, October 4, 2012

KATUNI ZA KONA YA MACHO KOMIKS

Face to Face After Fesbuk...

 

YANGA NA SIMBA HAKUNA MBABE

Timu za Yanga na Simba jana ziligawana point baada ya kutoka suluhu ya kufungana 1-1 katika mechi ya Ligi kuu iliyofanyika katika uwanja mpya wa taifa. (Picha kwa hisani ya Samsung Galaxy II) 

 Yanga wakishangilia bao la kusawazisha

Mdau kaka nanii akifuatilia mpambano.

Tuesday, October 2, 2012

USIKU WA LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO!


Mashindano ya Klabu bingwa Ulaya yanaendelea leo huku timu zikiingia katika mzunguko wa pili wa makundi yao kwa kucheza mechi za nyumbani na za ugenini. Ratiba kamili ya leo kwa hizsani ya ESPN ni kama ifuatavyo:

Tuesday, October 2, 2012
TimeHomeAwayStageVenue
21:45 GMT FC Nordsjælland  v  Chelsea Group E Farum Park
21:45 GMT Juventus  v  Shakhtar Donetsk Group E Juventus Stadium
21:45 GMT BATE Borisov  v  Bayern Munich Group F Dynamo Stadium, Minsk
21:45 GMT Valencia  v  Lille Group F Estadio Mestalla
21:00 GMT Spartak Moscow  v  Celtic Group G Luzhniki Stadium
21:45 GMT Benfica  v  Barcelona Group G Estadio da Luz
21:45 GMT CFR Cluj-Napoca  v  Manchester United Group H Stadionul Dr. Constantin Radulescu
21:45 GMT Galatasaray  v  Braga Group H Türk Telekom A

NI YANGA AU SIMBA KESHO?

Yanga SC ikiwa imewasambaratisha wapinzani wao wa jadi Simba SC katika vita ya usajili itakuwa inataka kuhamishia ubabe wake huo uwanjani swali je Yanga itaweza kufanya kile ilichokifanya nje ya uwanja? Kujibu swali hili hii inaifanya Mechi hii ya watani wa jadi kuwa Bonge la Mechi la kukata na shoka, lakini hii inaweza kuwa ni nje ya uwanja kutokana na matukio lukuki yaliyojitokeza hivi karibuni kati ya timu hizi mbili kongwe na hasimu.
                                             
      Mashabiki wa Yanga na Simba 

 Timu ya Simba


Tmu ya Yanga



Monday, October 1, 2012

MICHEZO YA SHIMIWI: HAZINA WAINGIA ROBO FAINALI KAMBA LEO

Timu ya kamba ya wanaume ya Wizara ya Fedha "Hazina Sports Club" leo imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali katika michezo ya SHIMIWI inayofanyika mjini morogoro baada ya kuivuta timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais. Picha kwa hisani ya Cox Kakoko.

Timu ikijiandaa

Timu ya hazina vitani.

Cox wa hazina akiwa mazoezini.

UMEWAHI KUISIKIA NGOMA YA BAIKOKO??

Ngoma Baikoko yenye asili ya mkoani Tanga ikichezwa kwa ustadi mkubwa. Maadili yetu yako wapi??

ENZI ZILE..

Pichani ni hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa amevalia mavazi ya kichifu na mkewe mama Maria Nyerere ikiwa kama moja ya kumbukumbu ya tulikotoka.