Hafla
ya kuwapongeza wanafunzi hao kutoka shule nane za serikali na mbili za
binafsi ilifanyika bungeni jana baada ya Bunge kutengua kanuni na
kuruhusu wanafunzi hao kuingia ukumbini.
Mbali
na fedha taslimu, wanafunzi hao walipewa zawadi za kompyuta ndogo
(Laptop) na cheti ambavyo walikabidhiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Pia kila shule iliyotoa mwanafunzi au wanafunzi bora imezawadiwa sh milioni moja.
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema jana kuwa
hafla hiyo inafanyika ili kuwaenzi na kuwapongeza wanafunzi waliofanya
vizuri.
No comments:
Post a Comment