SOUTHAMPTON YAKAMILISHA USAJILI WA EMMANUEL MAYUKA
Timu
ya Southampton inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza jana imethibitisha
kukubaliana mambo binafsi na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Zambia Chipolopolo Emmanuel Mayuka ili
kumsajili akitokea timu ya Young Boys inayoshiriki ligi kuu nchini Uswizi.
Mayuka, mwenye umri wa miaka 21,anahamia katika uwanja wa St. Marry unaomilikiwa na Southampton kwa ada ambayo haijatajwa bado ambayo itamfunga kilabuni hapo hadi msimu wa mwaka 2017. Mayuka ambaye ameshapata kibali cha kufanyia kazi nchini Uingereza anaweza kushuka dimbani katika mpambano wao dhidi ya Manchester United siku ya jumapili.
No comments:
Post a Comment