Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Friday, May 5, 2017

HIMID MAO AANZA KUFANYA MAJARIBIO DENMERK

NAHODHA Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, anaendelea na majaribio yake kwenye kikosi cha Randers inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark.

Himid tayari ameshafanya mazoezi mara mbili juzi na jana akiwa na kikosi cha wachezaji wa akiba wa timu hiyo, ambapo leo Jumatano alipewa mapumziko kabla ya kesho Ijumaa kuanza rasmi kujifua na kikosi cha kwanza cha Randers.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, umeeleza kuwa kiungo huyo nyota mkabaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, 24, yuko tayari kwa mara ya kwanza kucheza soka la kulipwa na kulipa kisogo soka la nyumbani kwa kuhakikisha anapata mkataba wa kusajiliwa na Randers.

#StayStrongHimidMao23 #GoodLuck

Wednesday, May 3, 2017

MBEYA CITY YAWASHANGAA YANGA KUTEMBEZA BAKULI

Kuna ujumbe nilikutana nao katika mitandao ya kijamii siku za hivi karibuni. Ukiusoma unafurahisha sana lakini umebeba ujumbe mzito sana.
Unasema wakati mwanamuziki Diamond Platnum amefanya hafla kubwa ya kuzindua biashara yake inayofahamika kama CHIBU PERFUME ambayo inauzwa shilingi laki moja na elfu tano (105000) kuna klabu kubwa hapa  nchini zimeshindwa kuweka utaratibu mzuri wa kujipatia hata 20000 kutokana na mauzo ya jezi za mastaa wao.

Maisha ndivyo yalivyo, kupanga ni  kuchagua. Diamond ameamua kuisimamisha Brand yake na wengine wameona kuwarudia wananchi wawachangie ndiyo maisha wanayostahili.

Diamond huyu ameamua kuingia kwenye ulimwengu mwingine tofauti na ule wa muziki. Ulimwengu wa kibiashara ambao unahitaji watu makini wanaoweza kuifanya biashara kusimama bila kuyumba. Sio kazi rahisi kama unavyoweza kufikiri unapoitazama ukiwa nje. Hata kama atakuwa anakutana na changamoto za hapa na pale ila kitu alichokifanya ni kikubwa sana.

Ubunifu wa aina hii ndio unaompa Cristiano Ronaldo jeuri ya kumiliki ndege binafsi na kuiishi dunia vile atakavyo.

Alishindwa Ngassa, Msuva nae licha ya kuwa na uhakika wa kukutana na mashabiki zaidi ya milioni kumi kwa mwaka bado anahisi hili ni kubwa sana kwake.

Kwa mazingira ya soka letu inawezekana suala hili likawa gumu kwa wachezaji wetu lakini hawana budi kubadilika maana dunia nayo imebadilika. Ni aibu sana mchezaji wa kizazi cha dunia ya leo kuishi katika dunia aliyoishi Sunday Manara au Athuman Machupa.

Sawa inawezekana wachezaji wanahofia ukubwa wa Brand zao lakini vipi kuhusu klabu nazo? Bado nazo zinahofia kuhusu ukubwa wa Brand?

Ukitafakari vizuri utakubaliaana na mimi hiki sio kikwazo kwa klabu zenye idadi kubwa ya mashabiki kama hizi za Kariakoo. Kama umeweza kuamini watu wanaweza kukuchangia fedha bure unashindwaje kuwatumia watu hao hao kuwa sehemu ya mtaji au soko lako?

Mpaka hapo unaweza kuamini na mimi tatizo kubwa linaloukwamisha mpira wetu kupiga hatua ni watu wanaouongoza mpira wenyewe.

Rasilimali watu ni kitu muhimu sana katika mustakabali wa maendeleo ya sekta yoyote. Ulishawahi kujiuliza kuwa Yanga wangeweza kuachwa na ndege nchini Algeria kama wangekuwa na mtaalamu wa masuala ya Logistics? Bila ya kuwa na watu sahihi unaweza kuwa na kila kitu lakini bado usifanikiwe.

Nairejea kauli ya Zeben Hernandez aliyekuwa kocha wa Azam fc wakati anaondoka alisema uwekezaji mkubwa bila watu sahihi ni sawa na bure.

Wanasema unapoona mdogo anamzidi mkubwa kwa busara na maarifa basi huitaji kufikiri sana kugundua hapo kuna tatizo.

Mbeya City anazidi kuyafanya tuliyotarajia kuyaona yakifanywa na kaka zake siku nyingi zilizopita.
Licha ya uchanga wao lakini wanaamini tayari nembo yao ni Brand inayoweza kuwapa fedha kutoka kwa wadhamini na kuwaondoa katika kundi la omba omba.

Mbeya City wametangaza rasmi wamesaini mkataba wa udhamini na kampuni ya vifaa vya michezo ya Sports Master.

Udhamini huo utaifanya kampuni hiyo kuwa mtengenezaji na msambazaji mkuu wa vifaa vyote vya michezo vitakavyokuwa vinatumiwa na klabu ya Mbeya City katika kipindi chote cha miaka miwili ya mkataba huo. 

Hii ina maana kuwa mbali na timu hiyo kunufaika na vifaa vya michezo vitakavyokuwa vikitengenezwa na kampuni hiyo pia itakuwa imeongeza chanzo kingine cha mapato kwa sababu kampuni ya Sports Master watalazimika kuilipa Mbeya City kutokana na nembo yao kuonekana kwenye jezi ya klabu hiyo.

Hii ni aina mojawapo kati ya zile aina za udhamini wa kwenye jezi ambapo makampuni mbalimbali ya Marekani na Ulaya kama Adidas na Nike huzilipa klabu kubwa fedha nyingi kwa ajili ya udhamini huu.

Kwa sasa Manchester united ndio wanaoongoza kwa kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na udhamini huo ambao wanaingiza kiasi cha Pauni milioni 75 kwa mwaka za Adidas wakifuatiwa na Chelsea watakaokuwa wakiingiza kiasi cha Pauni milioni 60 za Nike kwa mwaka kuanzia msimu ujao.

Ni hatua kubwa sana waliyopiga kama klabu kwa sababu wanaweza kuwa wameonyesha mfano kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kufanya hivyo. Ndio wameweza. 

Unafikiri Mbeya City wana nini cha kuwapa shavu kama hili zaidi ya viongozi makini?

Ndugu zetu wa Kariakoo wanalitambua hili?

Yupo mmoja anavaa jezi zinazotengenezwa na makampuni ya Nike na Kelme na mwingine akivaa zilizotengenezwa na kampuni ya Uhlsport.

Nisaidie hapa Je, klabu zinanufaika na chochote kutoka kwenye makampuni hayo kwa kuzitangaza nembo zao?

Jibu la swali hili ni jepesi sana, kama kinapatikana basi kinaishia tusikokujua mimi na wewe.

Mbeya City wameonekana kuwa makini sana kwa namna wanavyoingia katika masuala haya ya kibiashara.

Ukiachana na aina hii ya udhamini wa jezi ambao klabu hunufaika kutokana na kutangaza makampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo, pia kuna aina nyingine ya udhamini kupitia kwenye jezi ambapo klabu inaweza kuwa na wadhamini kadhaa kati ya mmoja au zaidi ambao bidhaa zao zitatangazwa kwenye jezi ya timu husika.

Mdhamini mkuu ndio hukaa sehemu ya mbele au sehemu ya tumbo wakati wale wadogo wakikaa nyuma mgongoni au kwenye fito za mikono.

Kwa aina hii ya udhamini Mbey city wanadhaminiwa na Bin Slum kupitia bidhaa yake ya RB Batteries ambayo nembo yake huonekana mbele ya jezi za timu hiyo. Pia Coca Cola ambao wanaidhamini timu hiyo kupitia jezi yao ambapo nembo yao huonekana kifuani kwa size ndogo juu ya nembo kubwa ya mdhamini mkuu.

Wanachokipata Mbeya City kutokana na ubunifu wao wa kutengeneza vyanzo vya mapato unawasaidia kuendesha timu bila ya kuwa na matatizo ya hapa na pale  ambayo yamekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa klabu zetu.

Licha ya udogo wa klabu yao lakini wamefanikiwa kuitumia nembo yao hiyo ndogo kunufaika nayo. Nawaza hapa ingekuwaje kama wao ndio wangekuwa na Brand kama zile za klabu fulani?

Wanahitaji nini zaidi ya kuwashangaa wasiojua ukubwa na thamani ya Brand za klabu zao? Sina budi kuwapongeza Mbeya city katika hili.

Ifike hatua tufikiri kutengeneza fedha za kuendeshea klabu zetu kutokana na nembo za klabu zenyewe. Bila kubadilika hatutaisha kutembeza bakuli kuomba misaada.

Klabu inahitaji kuwa na watu sahihi kila sekta ili kuendana na usasa. Hili linawahusu watu wa idara ya masoko ambao wanaweza kuhakikisha wanatengeneza mazingira mazuri ya kuwavutia wawekezaji na wadhamini ndani ya klabu.

Hivi kweli kwa ukubwa wa Simba, leo hii wanavaa jezi plain isiyokuwa na hata nembo ya mdhamini yeyote?
Najiuliza hapa wadhamini ndio wanakosekana au tatizo ni wao kutokujua thamani ya jezi yao.

Mbeya city hawana la kufanya zaidi ya kuendelea kuwashangaa na michango yao pamoja na madeni yao wanayoendelea kuyatengeneza kila siku maana unaweza kushangaa mmoja anamcheka mwenzie kwa kuamua kutembeza bakuli wakati wao wanaendesha timu kwa mikopo.

Thursday, February 9, 2017

BREAKING NEWS....... MAJIBU SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

GWAJIMA NAE AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI...
Mchungaji wa kanisa la Saa ya Ufufuo  Bw. Josephat Gwajima leo hii ameongea na waandishi wa habari akiwa na jopo l a maaskofu wake wasaidizi. Dhumuni la kuongea na waandishi hao ilikuwa ni kutoa ufafanuzi wa kuhusishwa kwake katika sakata linaloendelea nchini la kupambana na uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.




Akijibu maswali ya waandishi wa habari , Mchungaji gwajima alieleza kuwa anakubali kazi nzuri inayofanywa na Mh. Mkuu wa Mkoa lakini akisisitiza kuwa mkuu huyo hana uwezo wa kutawaLA na hivyo atatuma maombi kwa Mh. Rais ili apangiwe kazi nyingine.

Pia alisisitiza kuwa ataenda katika kituo cha kati cha polisi kuitikia wito siku ya leo na sio kesho kama alivyotakiwa na amesema yupo tayari kukaa ndani kwa miaka hata 40 kwa kuwa kama atabainika ana makosa.

Alipoulizwa kuhusu upatikanaji wa mali lukuki alizonazo, alieleza kuwa mali hizo zinatokana na jasho lake kwa kuwa amekuwa mhadhiri wa kimataifa wa dini huku akipata kiasi cha dola za kimarekani 1000 kwa kila kipindi. Pia alieleza kuwa kanisa lake lina kampuni ambayo huingiza pesa nyingi na yeye akiwa kama mkurugenzi wa kampuni hiyo. Alipoulizwa kuwa haoni sababu ya kuhusishwa na madawa ya kulevya imetokana na urafiki wake wa karibu na Waziri mkuu mstaafu aliyekuwa mgombea wa UKAWA, alijibu kuwa mambo ya uchaguzi yalishapita na sasa yeye anamuunga mkono Mh. Rais Magufuli.

Mwisho alisema kuwa wito wake aliusikia Redioni  lakini kwa unyenyekevu leo ataenda kuonana na kamanda wa polisi Siro katika kituo cha Polisi kati.

SAKATA LA VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA...MANJI AITIKIA WITO LEO POLISI

Mfanyabiashara mashuhuri nchini Yusuph Manji leo aliitikia wito wa mkuu wa Mkoa Mh. Makonda wa kuripoti katika kituo cha kati cha Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya. Hata hivyo Manji ambaye alitakiwa afike kituoni hapo siku ya Ijumaa amefika leo kituoni hapo huku sababu za kuwahi kwake zikiwa hazijulikani.

Picha na ripota wetu.

      Mashuhuda wakishuhudia




 Akiwasili....




Akiongea na baadhi ya Wadau

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA RC MAKONDA AWATAJA MBOWE, MANJI, GWAJIMA, IDD AZZAN...

Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ameongea na waandishi wa habari kuhusu muendelezo wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.



Mh. Paul Makonda amsema anataka wauzaji wa dawa za kulevya wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha. Pia ameasema vita vya dawa za kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani. “Kuna watu nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa, unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa”Alisema-RC Makonda. Aliendelea kwa kusisitiza


“Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya”-RC Makonda

“Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia”-RC Makonda

“Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi”-Makonda

“Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana”- Makonda

Tuesday, January 24, 2017

WARAKA WA MH. MBUNGE DKT. FAUSTINE NDUNGULILE KWA WAKAZI WA KIGAMBONI

*TAARIFA KUHUSU BARABARA TOKA DARAJA LA NYERERE NA TOZO ZA DARAJA*
Kwa muda mrefu nimekuwa nikipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na huduma isiyoridhisha kwenye Daraja la Nyerere linalounganisha Kigamboni na Kurasini.
Malalamiko ya wananchi yako kwenye maeneo makuu matatu:
1. Kutumika kwa madirisha machache ya kukatia tiketi. Daraja la Nyerere lina madirisha 14 ( Saba wakati wa kuingia na Saba wakati wa kutokea). Madirisha yanayotumika ni machache na hivyo kusababisha foleni isiyo na msingi.


2. Tozo za Daraja la Nyerere zipo juu sana hususan kwa magari ya abiria. Hali hii imepelekea Kigamboni kukosa ruti ndefu za kuelekea maeneo mengine ya Jiji la Dar Es Salaam. Gari la abiria linatozwa kati ya Tsh 5000-7000 kwa kila safari ambayo ni gharama kubwa sana kwa kutwa.
3. Kutokamilika kwa kipande kilichobaki toka Darajani hadi kwa Msomali.

Kama Mbunge wa Kigamboni nimekuwa nikifuatilia suala hili kwa karibu sana bila ya mafanikio. Tukumbuke kuwa Daraja la Nyerere lilizinduliwa tarehe 19.04.2016 na sasa ni zaidi ya miezi 9 hamna kinachoendelea na wahusika hawatoi majibu yanayotosheleza.

*HATUA NILIZOCHUKUA HADI HIVI SASA*
1. Mnamo tarehe 15.06.2016 nilimwandikia barua Waziri wa Ujenzi Mhe. Makame Mbarawa (Mb) kuhusiana na hoja hizi. Pamoja na kufuatilia zaidi ya mara kumi kwa simu, maongezi ya ana kwa ana na meseji, barua yangu haijajibiwa hadi hivi sasa (Angalia kiambatanisho).

2. Vile vile nilikutana na Mkurugenzi wa NSSF Prog Godius Kahyarara tarehe 3.10.2016 kuhusu hoja tajwa hapo juu. Aliahidi kuchukua hatua za haraka lakini hadi hivi sasa hakuna kilicofanyika.

3. Kwa kuwa usimamizi wa Daraja la Nyerere upo chini ya NSSF na kipande kilichobaki kitajengwa na NSSF, niliomba kukutana na Waziri anayesimamia taasisi hii. Nilikutana na Mhe. Waziri Jenista Mhagama (Mb) tarehe 3.12.2016 ofisini kwake. Pamoja na maelezo ya mdomo, nilimkabidhi barua ya malalamiko (Angalia kiambatanisho). Mheshimiwa Waziri aliahidi kuchukua hatua za haraka.
Tarehe 13.12.2016 nilipata nakala ya barua aliyoandika Mhe. Waziri Mhagama kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ili kupata maelezo na ufumbuzi wa hoja nilizotoa. Pamoja na kukumbushia Mhe. Waziri Mhagama hajanipatia majibu ya hoja zangu.


Aidha, maelezo niliyopata toka kwa Mkurugenzi wa NSSF wakati Waziri Mkuu anatembelea Kigamboni tarehe 04.01.2017 ni kwamba fedha zinazohitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande kilichobaki ni Tsh 24 Bilioni na alinihakikishia kuwa *FEDHA HIZO ZIPO.* *Michoro (design) ya barabara hiyo IMESHAKAMILIKA.* *Mkandarasi kwa ajili ya kazi hiyo YUPO.*

*Pamoja na NSSF kuwa na fedha ya ujenzi wa barabara hiyo, mkandarasi aliye tayari na michoro iliyokamilika, kumekuwa na kigugumizi ya lini kazi hii itaanza.*
Inasikitisha pia kuona Mawaziri hawajibu barua pamoja na kukumbushwa mara kwa mara.
Kinachoendelea sasa hakuna lugha nyingine ya kuielezea zaidi ya UZEMBE na KUTOWAJIBIKA.
Naleta taarifa hii kwenu wakazi wa Kigamboni ili nanyi mjue kinachoendelea. Ninakusudia kuyapeleka malalamiko yenu kwa mamlaka ya juu zaidi, baada ya mamlaka tajwa hapo juu kushindwa kupata ufumbuzi.

Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge
24.01.2017

Tuesday, January 17, 2017

MATOKEO YA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI 2016/ 2017 YATOKA


Tayari Serikali kupitia Baraza la mitiani NECTA imetangaza Matokeo ya kidato cha pili mwaka 2015  324,068 sawa na 89% kati ya wanafunzi 363,666 waliofanya mtihani wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu kwa mwaka 2016.
Matokeo yote unaweza kuyatazama hapa.


Pia unaweza kupata matokeo kwa kutuma SMS kwenda 15311. Kwa kufuata maelekezo yafuatayo..






































Send SMS to 15311
How to send SMS
  1. To get results: Write:
    matokeo*centre number*candidate number*exam type*exam year
    Example :
    matokeo*S1665*0041*k4*2014
    matokeo*M0110*0003*qt*2014
  2. To get rank: Write: rank*centre number*exam type*exam year Example : rank* S0101*k4*2014
Cost per SMS is Tshs 200/=
This service is only available for Tigo, Vodacom and Zantel subscribers.

Thursday, September 15, 2016

MBWANA SAMATTA: MTANZANIA WA KWANZA KUCHEZA LIGI YA UEFA EUROPA CUP

Mbwana Ally Samatta leo kama atafanikiwa kupangwa katika kikosi cha kwanza cha timu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji kinachotazamiwa kupambana na timu ya SK Rapid Wien leo mnamo saa 1 kamili usiku ataweka rekodi ya kuwa ni mchezaji pekee kutoka nchini Tanzania aliyewahi kucheza katika mashindano hayo ambayo ni ya pili kwa ukubwa barani Ulaya.  Na Mwandishi.
Pichani Mbwana Samatta akicheza kwenye Ligi ya Ubeligiji 

MBWANA SAMATTA: MTANZANIA WA KWANZA KUCHEZA LIGI YA UEFA EUROPA CUP

Mbwana Ally Samatta leo kama atafanikiwa kupangwa katika kikosi cha kwanza cha timu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji kinachotazamiwa kupambana na timu ya SK Rapid Wien leo mnamo saa 1 kamili usiku ataweka rekodi ya kuwa ni mchezaji pekee kutoka nchini Tanzania aliyewahi kucheza katika mashindano hayo ambayo ni ya pili kwa ukubwa barani Ulaya.  Na Mwandishi.
Pichani Mbwana Samatta akicheza kwenye Ligi ya Ubeligiji  

KONA YA LIVE FOOTBALL......LIGI YA UEFA EUROPA

Manchester united leo itakuwa kibaruani wakati itakapokuwa mgeni wa timu ya Feyenoord katika mji wa Rotterdam nchini Uholanzi... Mtanange huo unategemewa kupigwa mnamo saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Thursday, March 24, 2016

MAKONDA, MKUU MPYA WA MKOA MWENYE HOFU YA MUNGU

Mkuu mpya wa mkoa wa Dar-es-Salaam Mh. Paul Makonda ameonesha ni kiongozi shupavu na mwenye hofu ya Mungu. Hayo yamethibitika baada ya kuonekana akipata mibaraka kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Kiongozi wa Wakatoliki Kadinali Pengo.

Tuesday, March 15, 2016

EPL: LEICESTER CITY YAIBANJUA NEWCASTLE UNITED NA KUJIIMARISHA KILELENI

Timu ya soka ya Leicester City imeibanjua timu ya Newcastle kwa bao moja bila na kuendelea kuongoza ligi kuu ya England.
Katika mchezo huo, mshambuliaji kutoka Japani Ozaki aliipayia timu yake bao pekee la ushindi.

Monday, March 14, 2016

PICHA 7: MBWANA SAMATTA ALIVYONG'AA UBELIGIJI

Mshambuliaji wa timu ya KRC Genk ya nchini Ubeligiji Mtanzania Ally Mbwana Samatta ameendelea kuwika mwishoni mwajuma hili baada ya kuiongoza timu yake kuibanjua timu ya Oostvede FC kwa magoli 4-1 katika dimba lao la nyumbani.
Samatta alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake bao katika dk 23 baada ya kuunganisha kwa kichwa cha kuibia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto. Mpaka sasa Samatta ameshacheza mechi 6 na amekwisha funga jumla ya mabao 2.

Akiwahadaa wazungu.....

Samatta akifunga bao kwa kichwa

Samatta akipongezwa na wenzake..

Thursday, February 11, 2016

AJALI YA BASI LA SIMBA MTOTO

Basi la Kampuni ya SIMBA MTOTO lililokuwa linatokea Tanga asubuhi hii limepata ajali maeneo ya mkanyageni kwa kugongana na lori uso kwa uso inasadikiwa watu wengi wamefariki akiwamo Dereva na Kondakta wake. Picha na ripota wetu

 
 

UZEMBE WA KIVUKONI WAHATARISHA MAISHA YA WAKAZI WA KIGAMBONI

Wakazi wa Kigamboni asubuhi ya leo wamenusurika kuzama baharini baada ya kivuko cha MV Kigamboni kujaza abiria kupita kiasi na kusababisha kivuko hicho kushindwa kuinua milango yake. Picha na ripota wetu.

Kivuko kikijaza abiria zaidi ya uwezo wake
 
Mlango wa Kivuko ukigoma kufunga 
Abiria wakijitosa baharini kuokoa maisha yao..