Mkuu wa Mkoa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa
mkoa wa Dsm,ndugu Paul Makonda ameongea na waandishi wa habari kuhusu muendelezo
wa vita ya madawa ya kulevya ktk jiji la Dsm.
Mh. Paul Makonda amsema anataka wauzaji wa dawa za kulevya
wajulikane hadharani na hakuna sababu ya kuficha. Pia ameasema vita vya dawa za
kulevya vilianza muda mrefu kwa kufutilia hali ilivyo mitaani. “Kuna watu
nilitaka nikutane nao polisi, kuna tofauti kati ya kukamatwa na kuitwa,
unapoitwa unapewa nafasi ya kusikilizwa”Alisema-RC Makonda. Aliendelea kwa
kusisitiza
“Kampeni hii dawa ya dawa za kulevya si ya kufanyika kimyakimya tunataka hata
watoto wadogo wajue dawa hizi ni hatari kwa afya”-RC Makonda
“Asante kwa watu kama TID, nawapongeza kwa kukiri na kusema kuwa wanatambua
namna walivyoingia na kuomba serikali kuwasaidia”-RC Makonda
“Tumemaliza awamu ya kwanza vita ya dawa za kulevya, sasa hii ni awamu ya pili
ambayo itakuwa si nyepesi itakuwa na mawimbi mengi”-Makonda
“Awamu ya 2 ya vita ya dawa za kulevya tunaianza leo na tunaianza tukiwa
tumekamilika, nimekuwa kwenye operesheni usiku na mchana”- Makonda
No comments:
Post a Comment