GWAJIMA NAE AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI...
Mchungaji wa kanisa la Saa ya
Ufufuo Bw. Josephat Gwajima leo hii ameongea na waandishi wa habari akiwa na
jopo l a maaskofu wake wasaidizi. Dhumuni la kuongea na waandishi hao ilikuwa
ni kutoa ufafanuzi wa kuhusishwa kwake katika sakata linaloendelea nchini la
kupambana na uingizaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.
Akijibu maswali ya waandishi wa
habari , Mchungaji gwajima alieleza kuwa anakubali kazi nzuri inayofanywa na
Mh. Mkuu wa Mkoa lakini akisisitiza kuwa mkuu huyo hana uwezo wa kutawaLA na
hivyo atatuma maombi kwa Mh. Rais ili apangiwe kazi nyingine.
Pia alisisitiza kuwa ataenda
katika kituo cha kati cha polisi kuitikia wito siku ya leo na sio kesho kama
alivyotakiwa na amesema yupo tayari kukaa ndani kwa miaka hata 40 kwa kuwa kama
atabainika ana makosa.
Alipoulizwa kuhusu upatikanaji wa
mali lukuki alizonazo, alieleza kuwa mali hizo zinatokana na jasho lake kwa
kuwa amekuwa mhadhiri wa kimataifa wa dini huku akipata kiasi cha dola za
kimarekani 1000 kwa kila kipindi. Pia alieleza kuwa kanisa lake lina kampuni
ambayo huingiza pesa nyingi na yeye akiwa kama mkurugenzi wa kampuni hiyo.
Alipoulizwa kuwa haoni sababu ya kuhusishwa na madawa ya kulevya imetokana na
urafiki wake wa karibu na Waziri mkuu mstaafu aliyekuwa mgombea wa UKAWA,
alijibu kuwa mambo ya uchaguzi yalishapita na sasa yeye anamuunga mkono Mh.
Rais Magufuli.
Mwisho alisema kuwa wito wake
aliusikia Redioni lakini kwa unyenyekevu
leo ataenda kuonana na kamanda wa polisi Siro katika kituo cha Polisi kati.