Ndoto za Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kufuzu mzunguko wa pili wa kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil zilifutika jana kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar-es-Salaam baada ya kukubali lkipigo cha mabao 2-4 mbele ya Tembo wa Ivory Coast.
Katika mechi ya hiyo Stars walipata bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Amri Kiemba baada ya beki wa Ivory Coast kujichanganya. Bao la pili la kusawazisha lilifungwa na straika Thomas Ulimwengu kabla ya Ivory Coast kufunga bao yake kupitia kwa Yahya Toure aliyefunga mawili, Lacina Traore na Willfred Bony waliofunga goli moja kila mmoja. Tanzania licha ya kufungwa ilionyesha mchezo mzuri uliowabana Ivory Coast katika kipindi chote cha mchezo.
Umati wa wapenda kandanda ulioudhulia pambano.
No comments:
Post a Comment