Idara ya usimamizi wa mifumo ya kifedha katika Wizara ya Fedha leo walifanya tafrija fupi wizarani ya kumuuaga mtumishi mwenzao aliyestaafu kazi kitokana na sheria za kiutumishi Serikalini.
Thursday, June 27, 2013
Saturday, June 22, 2013
HARUSI YA YUSUPH MDOE KATIKA UKUMBI WA KIRAMUU MBEZI
Mdau Yusuph Mdoe jioni ya leo alimaliza wiki yake ya harusi kwa sherehe kubwa ya kukata na shoka iliyofanyika katika ukumbi wa Kiramuu Mbezi. Picha na Maria Sabega.
Friday, June 21, 2013
MDAU YUSUPH MDOE NA BI. SAFII WAFUNGA NDOA
Mdau Yusuph Mdoe jioni ya leo amefunga pingu za maisha na Bi. Safii katika msikiti wa Upanga na sherehe zitaendelea hadi kesho. Picha na mdau ngoda!
Wednesday, June 19, 2013
SENDOFF YA BI. SAFII RAMADHANI MSASANI CLUB
Sendoff ya Bi. Safii Ramadhani imefanyika usiku wa leo katika ukumbi wa Msasani Club na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali. Bi Safii anatarajia kufunga ndoa na Bw. Yusuph Mdoe Mwasala siku Ijumaa tarehe 21 na Sherehe siku inayofuta ya tarehe 22.
Monday, June 17, 2013
MATUMAINI YA TANZANIA KWENDA WORLD CUP BRAZIL 2014 YAYEYUKA
Ndoto za Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" kufuzu mzunguko wa pili wa kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2014 huko Brazil zilifutika jana kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar-es-Salaam baada ya kukubali lkipigo cha mabao 2-4 mbele ya Tembo wa Ivory Coast.
Katika mechi ya hiyo Stars walipata bao la kwanza katika dakika ya kwanza ya mchezo lililofungwa na Amri Kiemba baada ya beki wa Ivory Coast kujichanganya. Bao la pili la kusawazisha lilifungwa na straika Thomas Ulimwengu kabla ya Ivory Coast kufunga bao yake kupitia kwa Yahya Toure aliyefunga mawili, Lacina Traore na Willfred Bony waliofunga goli moja kila mmoja. Tanzania licha ya kufungwa ilionyesha mchezo mzuri uliowabana Ivory Coast katika kipindi chote cha mchezo.
Umati wa wapenda kandanda ulioudhulia pambano.
BOMU LAUA WAWILI ARUSHA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA
Mlipuko wa Bomu la kurushwa ulitokea Arusha na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeluhi wengine 70 wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Chama cha Chadema uliofanyika katika Uwanja wa Soweto Kata ya Kaloleni mjini Arusha. Mkutano huo ulikuwa ukiendeshwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha mjini Mh. Godbless Lema ambao wote wawili walinusurika. Serikali na uongozi mzima wa blog hii unalaani vikali vitendo hivi vya uvunjifu wa amani hapa nchini. Mungu ibariki Tanzania.
Mmoja kati ya watoto walioathirika na mlipuko
Subscribe to:
Posts (Atom)