Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" jana ilifanikiwa kuilaza timu ya taifa ya Morocco kwa idadi ya magoli 3-0 katika mchezo wa kutafuta nafasi ya kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia zinazotazamiwa kufanyika nchini Brazil mwakani 2014.
Magoli ya Taifa Stars yalifungwa na wachezaji wake wa kutegemewa wanaocheza soka la kulipwa katika klabu kongwe ya TP Mazembe ya Congo Mbwana Ally Samatta aliyefunga mara mbili na Thomas Ulimwengu.
Kikosi cha Stars kilicheza kwa kujiamini zaidi na mabadiliko yaliyofanya na kocha ya kumuingiza Ulimwengu katika kipindi cha pili ndiyo yaliyobadilisha sura ya mchezo.
Kikosi cha Taifa Stars
Thomas Ulimwengu.
Mbwana Ally Samatta akishangilia gili la pili
Wadau wakifuatilia mpambano huo kwa makini
Hata watoto nao walikuwepo!
No comments:
Post a Comment