USAFI KATIKA MAPENZI
KILA
mmoja wetu anafahamu nini maana ya usafi, lakini baadhi ya watu
wamekuwa hawatilii maanani, hawana habari, hawajali pia wapo wengine
hawajui kabisa waanzie wapi kuwa wasafi. Na ile kauli ya kwamba mapenzi hayana chafu yamepitwa na wakati kutoka na kuongezeka kwa magonjwa mbali mbali siku hizi.
Mapenzi yanahusisha mambo na maungo mbalimbali
kama vile miguu (legs), miguu ya kukanyagia (feet) na kucha zake,
mikono, viganja ikiwa ni pamoja na kucha zake,macho, pua, midomo ya nje
(lips), kinywa, nyayo, makalio, alafu ndio zinafuata sehemu nyeti.
Maungo hayo yote yanamaana na umuhimu wake katika swala zima la mapenzi
hasa yakitumiwa ipasavyo na yakiwekwa katika hali ya usafi, vinginevyo
utampoteza mpenzi wako au kuharibu uhusiano wenu mzuri mlionao.
Usafi ninaouzungumzia hapa sio ule wa kuoga na kupaka Manukato
(perfum)/Lotion/mafuta, kufua/kunyoosha nguo pekee bali ni usafi ule wa
ndani ambao baadhi ya wanawake hufundishwa tangu wakiwa na umri mdogo.
Hali kadhalika wanaume pia hufundishwa jinsi ya kujisafi baadhi ya
maeneo ya miili yao, lakini inasikitisha kuwa wanaume wengi hawajali
kabisa usafi uwe ni ule wa kawaida au ule wa kunako nyeti.
Wapo
baadhi ya wanume na wanawake ambao hupenda sana kulambwa lambwa katika
maeneo Fulani ya miili yao wakidai kuwa ndio inayowaongezea nyege,
lakini cha kusikitisha ni kuwa watu hawa hawajali/hawatunzi maeneo hayo
na badala yake kutegemea mwanamke amshughulikie.
Leo
nitazungumzia utunzaji wa kinywa na kunako majaaliwa nitaelezea umuhimu
wa kila kiungo nilichokitaja hapo awali na utunzaji wake.
*Sugua meno yako kila siku asubuhi na jioni, ikiwezekana kila baada ya
kula chakula. Anza kwa kusugua meno pande zote juu, chini, katikati na
pembeni, hakikisha kila pande unatumia dakika kumi.
*Safisha
mswaki wako na usugue ulimi wako sehemu ya katikati na pembeni rudia
mpaka ukitema mate yasiwe na mrendamrenda, kisha suuza na maji ya
vuguvugu.
*Ikiwa “unaasili” ya kuwa na nyuzinyuzi katika kinywa
yaani ukiongea/kucheka/ kupiga miayo n.k kunatokea mate yaliyoungana
mithili ya uzi, hali hiyo hakika hutia kichefuchefu.
Unachotakiwa kufanya kila baada ya kula ni kutafuna kipande cha
limau/ndimu/mbilimbi/mdalasini ambayo itasaidia kukata mate au tafuna
bazoka zenye MINT (Bongo zipo na zinauzwa Tsh.2,000 kwa paketi) ambazo
hazijaongezewa sukari ili kuepusha harufu mbaya ya kinywa na meno yako
yasioze.
Usikukose kutembelea hapa ili jue jinsi yakujiswafi
maeneo mengine kwa njia ya asili ambayo si ghali kwa watanzania wengi na
ile ya kileo ambayo tunawaachia wenye kuweza.
Siku njema. (Makala na Oooooh itie Yote)