Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" jana ilifanya maajabu kwa kuifunga timu ya taifa ya Cameroon mabao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa taifa mjini Dar-es-Salaam, Tanzania.
Goli la Tanzania lilifungwa na mshambuliaji wake anayecheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya nchini DRC Congo katika dakika ya 88 ya mchezo kutokana na krosi iliyopigwa na beki Erasto Nyoni.
Mshambuliaji wa Taifa Stars Mbwana Ally Samatta akifunga goli
No comments:
Post a Comment