TAARIFA YA TAHADHARI: TSUNAMI LA BAHARINI KUTOKEA LEO JIONI PWANI YA MTWARA NA DAR
Taaria iliyotolewa na Malmaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Tsunami kubwa linatarajiwa kutokea katika Pwani ya Mtwara na Dar es Salaam.
Taarifa iliyotangazwa katika vyombo vya habari imesema mawimbi makali zaidi yanatarajiwa kutokea Pwani ya Mtwara na Dar es Salaam kwa kiasi, kuabzia 211 11.30 jioni.
TMA imesema Tsunami hiyo inatokana na tetemeko lililotokea chini ya Bahari Hindi leo asubuhi na kwamba kutokana na umbali wa eneo lililkotokea tetemeko hilo athari zake zinakadiriwa kufika Tanzania muda huo wa saa 11. 30 jioni.
Kufuatia hali hiyo tahadhali zote zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kusitishwa usafiri wa baharini na vyombo vingine vya uvuvi.
Kwa mujibu wa TMA vyombo vitakavyokutwa vipo majini saa 11.30 vinashauriwa kuendelea kuweko huko visije kwenye pwani na pia vile ambavyo havijaingia baharini visingie.
Wale wanaoishi kandoni mwa bahari wametakiwa kuhama kwa muda kujihami na madhara. hata hivyo taarifa haikusema ni umbali gani ambao utakuwa salama na athari hizo kutoka eneo la bahari
No comments:
Post a Comment