Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Sunday, April 15, 2012

Kili Music Awards 2012....

HAWA NDO WASHINDI WA KILI MUSIC AWARDS 2012.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa George Meneja wa bia ya Kilimanjaro.

1. WIMBO BORA WA RAGGAE.
-ARUSHA GOLD BY WARRIORS FROM EAST.

2. WIMBO BORA WA DANCE HALL.
- MANENO MANENO BY QUEEN DARLIN.

3. WIMBO BORA WA ZOUK RHUMBA.
- DUSHELELE BY ALI KIBA.

4.BORA WENYE VIONJO VYA KIASILI.
- VIFUU UTUNDU BY A.T-

5. WIMBO BORA WA TAARABU.
- NANI KAMA MAMA BY MASHAUZI CLASSIC ( AISHA MASHAUZI).

6. WIMBO BORA WA KISWAHILI.
- DUNIA DARAJA BY TWANGA PEPETA-

7. WIMBO BORA WA AFRO POP.
- HAKUNAGA BY SUMA LEE-

8. WIMBO BORA WA R&B.
- NUMBER ONE FAN BY BEN PAUL-

9. WIMBO BORA WA HIP HOP.
- MATHEMATICS BY ROMA-

10. MSANII BORA ANAECHIPUKIA.
- OMMY DIMPOZ (NAI NAI SINGER).

11. RAPA BORA WA BAND.
- KALIJO KITOKOLOLO-

12. MSANII BORA WA HIP HOP.
- ROMA MKATOLIKI-

13. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA.
 - NAI NAI BY OMMY DIMPOZ FT. ALI KIBA-

14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI.
-KIGEUGEU BY JAGUAR-

15. MTUMBWIZAJI BORA WA KIKE.
- KHADIJA KOPA-

17. MTUNZI BORA WA MWAKA.
    - DIAMOND-

16. MTUMBWIZAJI BORA WA KIUME
- DIAMOND-

18. MTAYARISHAJI BORA WA MAPIGO YA MUZIKI.
- MANEKE-

19. VIDEO BORA YA MWAKA.
- MAWAZO BY DIAMOND-

20. WIMBO BORA WA MWAKA.
      - HAKUNAGA BY SUMA LEE-

21. HALL OF FAME.
     -  TAASISI JKT-

22. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
      - KING KIKII-

23. HALL OF FAME KWA MTU BINAFSI.
     - DR. REMMY ONGALA-

24. MWIMBAJI BORA WA KIKE.
     - LADY JAY DEE-

25. MWIMBAJI BORA WA KIUME.
                                                     - BARNABA-

 Habari katika Picha ni kama ifuatavyo....

Mwanamuziki Diamond (katikati) akipiga picha na mama yake wa pili kutoka (kushoto) na Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka


Watoto wa Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa wakishuka jukwaani baada ya kumtunza mama yao wakati alipokuwa akitumbuiza katika hafla hiyo.

 Mkali wa Rap, Profesa Jay (kulia) na Meneja wa kundi la TMK Family Mkubwa Fella  wakimkabidhi tuzo Roma Msanii wa muziki wa Hiphop aliyejishindia tuzo ya msanii bora wa Hiphop.

 Mchekeshaji Steve Nyerere akipozi na Sinta mwigizaji wa zamani.

 P. Funk (kulia) akipozi na msanii wa muziki wa Hiphop Jay Mo.

Mwimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akipokea tuzo ya wimbo wa kiswahili  (bendi) uitwao Dunia Daraja.

Muigizaji wa Kundi la Komedy, Mjuni a.k.a Mpoki ambaye alikuwa ni mshereshaji wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Queen Darleen akishukuru kupokea tuzo.
Picha kwa hisani ya Sufiani Blog.
 

Wednesday, April 11, 2012

Tahadhariiii!

TAARIFA YA TAHADHARI: TSUNAMI LA BAHARINI KUTOKEA LEO JIONI PWANI YA MTWARA NA DAR

Taaria iliyotolewa na Malmaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema Tsunami kubwa linatarajiwa kutokea katika Pwani ya Mtwara na Dar es Salaam.
      Taarifa iliyotangazwa katika vyombo vya habari imesema mawimbi makali zaidi yanatarajiwa kutokea Pwani ya Mtwara na Dar es Salaam kwa kiasi, kuabzia 211 11.30 jioni.
   TMA imesema Tsunami hiyo inatokana na tetemeko lililotokea chini ya Bahari Hindi leo asubuhi na kwamba kutokana na umbali wa eneo lililkotokea tetemeko hilo athari zake zinakadiriwa kufika Tanzania muda huo wa saa 11. 30 jioni.
     Kufuatia hali hiyo tahadhali zote zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kusitishwa usafiri wa baharini na vyombo vingine vya uvuvi.
     Kwa mujibu wa TMA vyombo vitakavyokutwa vipo majini saa 11.30 vinashauriwa kuendelea kuweko huko visije kwenye pwani na pia vile ambavyo havijaingia baharini visingie.
      Wale wanaoishi kandoni mwa bahari wametakiwa kuhama kwa muda kujihami na madhara. hata hivyo taarifa haikusema ni umbali gani ambao utakuwa salama na athari hizo kutoka eneo la bahari

KANUMBA'S DEATH....

ELIZABETH ‘Lulu’ MICHAEL WAS BROUGHT TO COURT TODAY

 Elizabeth Michael on Good Friday before Kanumba's death

We have received unconfirmed reports that actress Lulu was brought to court this morning to face charges for her involvement in the death of boyfriend and actor Steven Kanumba. Sources say she was brought to the Kisutu Resident Magistrate’s Court earlier today where Judge Augustino Mmbando read her charges, however Lulu could not reply to them since this court does not handle murder trials.

Sources say that the case is scheduled to be heard o the 23rd of April, and that Lulu was swiftly brought in and out of court under heavy security.

Tuesday, April 10, 2012

Breaking Newsss!!!!

WEMA SEPETU AZIMIA NA KUKIMBIZWA HOSPITAL WAKATI WA MAZISHI YA KANUMBA




MUIGIZAJI MAARUFU WEMA SEPETU AKIWA AMEBEBWA NA WASAMALIA WEMA MARA BAADA YA KUZIRAI WAKATI WA MAZISHI YA MSANII kANUMBA! INASEMEKANA AMEPELEKWA HOSPITAL KWA MATIBABU ZAIDI.....
(Habari na Dar-es-Salaam yetu Blog)

Kwa heri Kanumba.....

MATUKIO YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KANUMBA

Viongozi wakiwasili Leaders


Kwaya ya Injili ikiomboleza

Watoto walioigiza na Ancle JJ nao wakiingia.

Dada wa Marehemu akiwa amezimia.

Mama wa marehemu Stevin Kanumba akipungia mikono waombolezaji

Mwili wa marehemu ukiwasili




Huduma ya kwanza

Makamu wa Rais

Mama Salma Kikwete


Sugu


Monday, April 9, 2012

..Safari ya milele ya Steven.....



RATIBA YA MAZISHI YA KANUMBA

Mwili wa marehemu Steven Kanumba utachukuliwa kwa msafara kutoka Hospitali ya Taifa, Muhimbili saa 2:30 asubuhi. Utapitishwa Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga.


Wito unatolewa kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa 2:00 asubuhi, wakijipanga kando ya Barabara za Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi ili wautolee heshima mwili wa Kanumba wakati ukitolewa Muhimbili kwenda Leaders Club.


Saa 3:30 asubuhi, mwili wa Kanumba utapokelewa Viwanja vya Leaders, ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.


Saa 4:00, itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo itachukua dakika 60, saa 5:00 kitakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali.


Saa 6:00 mchana, ratiba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9:00 alasiri na baada ya hapo, utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka Makaburi ya Kinondoni, msafara ukipita Barabara ya Tunisia, utakatisha Barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini.


Saa 10:00 alasiri, mazishi yatafanyika kwa kufuata utaratibu wa imani ya marehemu.


Kamati ya Mazishi inatoa wito kwa watu watakaohudhuria shughuli ya kumzika ndugu yetu Kanumba, kuja na maua ili kumuaga kwa heshima.

Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba.

Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe.



                                            K.N.Y GABRIEL MTITU

                                   MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI


 

Saturday, April 7, 2012

Breaking News...... Steven Kanumba afariki Dunia!

MASKINI KANUMBA...MAJONZI NCHI NZIMA !

Ni alfajiri kabisa kama saa 12 hivi watu wengine wakiwa ndio wanaamka na wengine wakienda kulala na kupata mshtuko wa kuondokewa na kipenzi chao kwenye tasnia ya filamu hapa bongo Steven Kanumba nyumbani kwake Sinza Vatican. Chazo kinasema Kanumba alitoka kuoga na kumkuta Lulu ambaye inasemekana ni wapenzi akiongea na simu ndipo hapo ugomvi ulipoanzia mpaka kanumba kujikuta akidondokea kisogo na kutokwa na damu nyingi. 
 
Kwa sasa msanii wa kike Lulu anashikiliwa na police kwa maelezo zaidi, mdogo wake kanumba athibitisha uwepo wa lulu wakati Kanumba akipatwa na matatizo yaliyosababisha kifo chake, anasema wawilihao walikuwa na mabishano makubwa kabla ya Lulu hajatoka ndani kumuita na kumwambia kwamba Kanumba amedondoka na anatokwa na mapovu mdomoni.



HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
 
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na  sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
 
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
 
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.
 
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
 
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
 
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
 
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.