Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Thursday, July 24, 2014

MKE WA MTU SUMU! JAMAA APIGWA NA SULULU KATIKA FUMANIZI

 
Samahani kwa picha zitakazofuatia katika habari hii. Jamaa mmoja mkoani Mara amenusurika kupoteza maisha baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu kitendo kilichopelekea kupigwa Sululu kichwani na mmiliki wa mke huyo. Habari zilizotufikia zimedai kuwa baada ya kupigwa na sululu hilo mtuumiwa aliwahishwa hospitali kwa matibabu. Hadi tunapata habari hizi hatukuwaeza kujua hali halisi ya mhanga huyo!

 
Sululu likiwa limenasa katika kichwa

Madaktari wakijitahidi kuokoa maisha ya mtuhumiwa

 
Baada ya kushonwa 

Wednesday, July 2, 2014

BREAKING NEWS!!! MAJAMBAZI YAFANYA JARIBIO LA KUTOROSHA WAFUNGWA

Habari za kuaminika zimeifikia blog hii leo mchana zikisema majambazi yasiyojulikana leo katika maeneo ya Mikocheni karibu na TMJ Hospital yaliirushia risasi basi lililokuwa limebeba wafungwa katika jitihada za kutaka kuwatorosha wafungwa. Hadi tunapata habari hizi ilikuwa haijulikani kama kuna yeyote aliyejeruhiwa au kupoteza maisha katika shambulio hilo. Hali kadharika haijulikani kama kuna mfungwa yeyote aliyetoroshwa hadi sasa!


 
 
 Watu wakiwa wamekusanyika kwenye tukio

 
Gari lililobeba wafungwa likiwa limevunjwa vioo
 

Thursday, June 26, 2014

MBUNGE WA KIGAMBONI DR. F. ANDUNGULILE AONGEA NA TANESCO KUHUSU KERO ZA UMEME

Mrejesho wa suala la umeme kwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kigamboni

Siku ya Jumatatu tarehe 23.06.2014 nilifanya mkutano na uongozi wa Tanesco ngazi ya Mkoa wa Temeke na Wilaya ya Kigamboni. Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na:

Kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme Umeme mdogo kwa baadhi ya maeneo Uunganishaji wa umeme kwa wateja wapyaMiradi mipya ya umeme kwa Jimbo la Kigamboni

1. KUKATIKA KWA MARA KWA UMEME JIMBO LA KIGAMBONI

Umeme unaopatikana kwa wateja wa Jimbo la Kigamboni unatoka sub-station ya Ilala. Umeme huu pia husambazwa kwa maeneo ya Temeke, Mbagala na Mkuranga. Kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji pamoja na uchakavu wa miundombinu, kumekuwa na ukatikaji wa umeme mara kwa mara.

Tanesco walinieleza kuwa hatua ambazo wanachukua kuondoa tatizo hili ni pamoja na maboresho ya miundombinu, kusafisha njia unaopita umeme huo kwa kukata miti na matawi na kujenga sub-station mpya maeneo ya Mbagala. Kukamilika kwa sub-station ya Mbagala utapunguza utegemezi uliopo sasa kwa sub-station ya Ilala. Kazi ya ujenzi wa sub-station mpya unatarajia kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.

2. UMEME MDOGO KWA BAADHI YA MAENEO (LOW VOLTAGE)

Kuna baadhi ya maeneo kama vile Kijichi na Magogoni kumekuwa na tatizo la umeme mdogo. Tanesco walinitaarifu kuwa kuna mpango wa kufanya “voltage improvement” kwa kufanya “phase addition” na kuongeza transfoma nyingine mbili maeneo ya Magogoni. Transfoma zipo na ninatarajia kazi hii itaanza hivi karibuni. Kwa upande wa Kijichi, pamoja na “voltage improvement” bado kutakuwa na tatizo. Suluhu ya kudumu itakuwa kukamilika kwa sub-station ya Mbagala.

Tulikubaliana kuwa kazi hii iwe imekamilika ndani ya miezi mitatu ijayo.

3. UMEME KWA WATEJA WAPYA

Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi toka kwa wananchi wengi ambao wamekuwa wakisubiri muda mrefu kupata huduma ya umeme. Malalamiko yamekuwa yakitoka Kibada, Gezaulole, Toangoma, Saku, Rufu na Kiponza.

Uongozi wa Tanesco ulinihakikishia kuwa maandalizi yamekamilika kwa ajili ya usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya Kibada (blocks 14,15,16,17,18,19,20).  Waliahidi kukamilisha kazi hii ifikapo mwezi Septemba 2014.

Niliwataka ndani ya wiki tatu (3) kunipa mikakati yao ya kuwapatia umeme wananchi walioomba toka maeneo ya Gezaulole, Mbwamaji, Kizani, Mwera, Kibada(blocks zilizobaki), Ponde, Goroka Kalakala, Masaki na  Malela. Uongozi wa Tanesco uliahidi kufanya hivyo kwani miradi hii imeshatengewa Bajeti zake. Pia, Tanesco haina uhaba wa vifaa vya kuunganisha umeme kwa sasa.

4. MIRADI MIPYA YA UMEME JIMBO LA KIGAMBONI 

Uongozi wa Tanesco ulinitaarifu kuwa maombi yangu ya kutaka Kata za Kimbiji na Pemba Mnazi kuingizwa kwenye mradi wa Umeme Vijijini (REA) yamekubaliwa na sasa kata hizi zitaanza kupata huduma ya umeme.

Kama nilivyoeleza hapo juu, umeme wa sasa kwa Jimbo la Kigamboni hutoka Ilala, ujenzi wa Sub-Station ya Mbagala unaendelea na unatarajia kukamilika mwezi Disemba, 2014. Kukamilika kwa kituo kutafanya baadhi ya maeneo ya Jimbo la Kigamboni kujitegemea kwa huduma ya umeme na pia kuondokana kukatika katika mara kwa mara kwa umeme kama ilivyo sasa.

Vile vile Tanesco ipo kwenye mchakato wa kutafuta eneo katika Tarafa ya Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa sub-station mpya. Katika mwaka huu wa fedha hakuna fedha iliyotengwa kwa mradi huu. Lengo ni kuingiza ujenzi wa sub-station kwenye bajeti ijayo.

Aidha, niliwataka uongozi wa Tanesco kufanya maandalizi ya awali kujua gharama za kufikisha umeme katika maeneo ya Mwasonga, kata ya Kisarawe II ili makisio haya yaingizwe bajeti ya mwakani.Tulikubaliana zoezi hili kufanyika ndani ya miezi mitatu.

5. HITIMISHO 

Shirika la Tanesco halina uhaba wa vifaa kwa sasa. Niliwataka Tanesco Kigamboni kuandaa mpango kazi wa usambazaji wa huduma ya umeme kwa wateja wapya  ambayo itanisaidia kufuatilia utendaji kazi wao; kuboresha mawasiliano na mahusiano na wateja pindi umeme unapokatika au pale wateja wanapofika kuuliza kuhusu hatma ya maombi yao. Kwa vile, Tanesco ina uhaba wa vikosi vya kuunganisha umeme kwa wananchi, niliwashauri waangalie uwezekano wa kutumia wakandarasi binafsi (outsourcing) baadhi ya kazi hizi.

Kwa wananchi wa Kibada, Toangoma na Gezaulole kwa maeneo mliyoniletea orodha zenu, ndani ya siku 21 nitawapatia majibu ya lini maeneo yanatarajiwa kufikiwa. Aidha, nashauri maeneo husika kuunda kamati ambazo zinashirikiana nami katika ufuatiliaji.

Nawasilisha

Dkt Faustine Ndugulile (MB)

Mbunge Kigamboni

Friday, June 20, 2014

UINGEREZA YAPIGISHWA KWATA NA URUGUAY

Mshambuliaji wa timu ya Liverpool Luis Suarez jana aliongoza maangamizi ya kwa timu ya Uingereza dhidi ya timu ya taia lake la Uruguay.
Suarez alikua muiba mchungu kwa Uingereza baada ya kufunga mabao yote mawili na hivyo kuizamisha kwa mabao 2-1.

Suarez akishangilia bao lake la kwanza 
Suarez akifunga bao la pili 
Luis Suarez akishangilia bao la pili na wenzake 
Luis Suarez akiwasikiliza mashabiki kwa furaha 

Thursday, June 19, 2014

IVORY COAST YABAMIZWA NA COLOMBIA

Timu ya taifa ya Ivory Coast leo imefungwa mabao 2-1 na timu ya Colombia katika mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea nchini Brazil.

Yaya toure wa Ivory Coast akifanya yake 
 
 




  Gervinho na Tiote wakipongezana

Yaya Toure akisikitika baada ya mchezo kumalizika 
Rodriguez wa Colombia akishangilia na wenzake 

AJALI DARAJA LA KINYEREZI

Ajali mbaya ya kuanguka kwa lori kubwa lililokuwa limebeba contena lenye urefu wa 40ft imetokea katika daraja la kinyerezi na kusababisisha uharibifu mkubwa wa daraja hilo. Ajali hii imesababishwa na uzito mkubwa wa mzigo uliokuwa umebebwa na lori hilo.

Lori likiwa limepinduka  
 
Kontena likiwa linazama kwenye maji 

WORLD CUP 2014

SPAIN NA CAMEROON ZATUPWA NJE 
Timu za taifa za Spain na Cameroon zimeondoshwa katika mashindano ya World Cup yanayoendelea baada ya kukung'utwa mabao 2-0 na 4-0 na timu za Chile na Crotia walizopambana nazo. Habari zaidi kama Picha zonavyoonyesha.

 Chile forward Eduardo Vargas celebrates scoring the opener at the Estadio do Maracana




 Chile midfielder Charles Aranguiz scores in the 43rd minute to give the South Americans a two-goal lead at half-time.
Chile forward Eduardo Vargas celebrates scoring the opener at the Estadio do Maracana

 Olic makes a tackle on Cameroon's Benjamin Moukandjo.







Spain react after giving up a second goal to Chile at the Maracana.

Wednesday, March 19, 2014

Kutoka bungeni....

HOTUMA YA JAJI WARIOBA YAFUNIKA

 

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba jana aliliteka Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, alipowasilisha Rasimu ya Katiba na kushangiliwa katika maeneo mengi nyeti na kupigiwa kelele katika vipengele vichache vya uraia na ardhi. 

Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu – Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema Warioba katika hotuba yake ya aya 191.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji Warioba alisema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.
“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,” alisema.
Alisema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya Tanzania Bara tu.
“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,” alisema.
Warioba alishangiliwa tena na baadhi ya wajumbe aliposema: “Muundo wa Serikali Tatu haupunguzi uimara wa Muungano na muungano huo ni wa nchi mbili kwa manufaa ya wananchi, “Faida kubwa iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita ni kuungana kwa wananchi.”
Waliotoa maoni
Kuhusu idadi ya waliotoa maoni, alisema watu wengi waliotoa maoni kuhusu Muungano walijikita katika muundo wake kama njia ya kuondoa kero,” alisema.

Alifafanua kwamba Tanzania Bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu muungano na kati ya hao, 27,000 walizungumzia muundo wake.
Kwa Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwenye suala la Muungano na kwamba kati ya watu 38,000 waliotoa maoni kuhusu Muungano, 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wake.
“Wananchi waliotoa maoni kuhusu muundo wa Muungano kwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 13 walipendelea Serikali moja, asilimia 24 Serikali mbili na asilimia 61 waliendekeza Serikali Tatu” alisema na kuongeza;
Utafiti wa Tume
Alisema kuwa baada ya kuchanganua sababu mbalimbali zilizotolewa na makundi mbalimbali tume hiyo ilianza kufanya utafiti wa kina kuhusu muundo wa muungano na matatizo yake tangu ulipoundwa Aprili 26, 1964, na kutaja tume zilizopendekeza Serikiali tatu.
Alizitaja tume ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka 1993, kundi la Wabunge 55 kutoka Tanzania Bara (G 55) waliopeleka bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na Tume ya Jaji Kisanga.
Changamoto Serikali Tatu
Kuhusu Serikali Tatu ambao chama tawala (CCM), kimekuwa kinaupinga kwa udi na uvumba, Jaji Warioba alisema muundo huo utakuwa na changamoto zake, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama ingawa hazitakuwa kubwa kama inavyofikiriwa.
“Gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika eneo la ulinzi na usalama, yaani jeshi la wananchi, polisi, usalama wa taifa na mambo ya nje. Gharama hizo hazibadiliki, zinabaki zile zile bila kujali kama ni muundo wa Serikali mbili au Serikali tatu,” alisema.
Alisema tangu Muungano uundwe, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimekuwa zikiongeza wizara, mikoa, wilaya na taasisi mbalimbali za kiutawala ili kuleta ufanisi na hivyo kuongeza matumizi ya Serikali.
“Tume imependekeza kodi ya bidhaa iwe ya Muungano, pia mapato yasiyo ya kodi, mikopo na michango ya nchi washirika. Ushuru wa bidhaa utakidhi sehemu kubwa ya gharama za muungano,” alisema na kuongeza:
“Kwa upande wa matatizo ya kiutendaji, tume imependekeza muundo wa Serikali tatu ujengwe kwenye misingi minne ya utendaji – muungano wa hiyari, ushirikiano, mshikamano na kutegemeana.

Thursday, January 23, 2014

JUAN MATA KAMILISHA DILI LA KUJIUNGA NA NA MAN UNITED


Club ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imekubali ofa ya paund za kiingereza £37million kutoka kwa Club pinzani ya Manchester United, kama ada ya uamisho wa kiungo mshambuliaji Juan Mata na mapema iwezekanavyo mchezaji huyu wa kimataifa wa Hispania ataruhusiwa kujiunga na Manchester United kukamilisha hilo dili hili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.



Mata atachukua vipimo siku ya Alhamisi kabla ya kukamilisha uamisho wake, ambao utamfanya kupata mara mbili ya mshahara aliokuwa anaupata chelsea kwa wiki.
Juan Mata

Wednesday, January 22, 2014

MANAIBU WAZIRI WIZARA YA FEDHA WAINGIA OFISINI LEO

Manaibu waziri wapya wa wizara ya fedha leo wamewasili katika ofisi zao tayari kuanza kazi baada ya kuapishwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete siku chache zilizopita. Manaibu hao Mh.Mwigulu Nchemba na Adam Malima walilakiwa na wafanyakazi wlte wa wizara ya fedha.
Mh. Mwigulu Nchemba.
Mh. Adam Malima
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha.