Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Thursday, June 19, 2014

AJALI DARAJA LA KINYEREZI

Ajali mbaya ya kuanguka kwa lori kubwa lililokuwa limebeba contena lenye urefu wa 40ft imetokea katika daraja la kinyerezi na kusababisisha uharibifu mkubwa wa daraja hilo. Ajali hii imesababishwa na uzito mkubwa wa mzigo uliokuwa umebebwa na lori hilo.

Lori likiwa limepinduka  
 
Kontena likiwa linazama kwenye maji 

WORLD CUP 2014

SPAIN NA CAMEROON ZATUPWA NJE 
Timu za taifa za Spain na Cameroon zimeondoshwa katika mashindano ya World Cup yanayoendelea baada ya kukung'utwa mabao 2-0 na 4-0 na timu za Chile na Crotia walizopambana nazo. Habari zaidi kama Picha zonavyoonyesha.

 Chile forward Eduardo Vargas celebrates scoring the opener at the Estadio do Maracana




 Chile midfielder Charles Aranguiz scores in the 43rd minute to give the South Americans a two-goal lead at half-time.
Chile forward Eduardo Vargas celebrates scoring the opener at the Estadio do Maracana

 Olic makes a tackle on Cameroon's Benjamin Moukandjo.







Spain react after giving up a second goal to Chile at the Maracana.

Wednesday, March 19, 2014

Kutoka bungeni....

HOTUMA YA JAJI WARIOBA YAFUNIKA

 

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba jana aliliteka Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, alipowasilisha Rasimu ya Katiba na kushangiliwa katika maeneo mengi nyeti na kupigiwa kelele katika vipengele vichache vya uraia na ardhi. 

Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu – Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano,” alisema Warioba katika hotuba yake ya aya 191.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji Warioba alisema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.
“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya kufanya mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa nchi moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,” alisema.
Alisema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya Tanzania Bara tu.
“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,” alisema.
Warioba alishangiliwa tena na baadhi ya wajumbe aliposema: “Muundo wa Serikali Tatu haupunguzi uimara wa Muungano na muungano huo ni wa nchi mbili kwa manufaa ya wananchi, “Faida kubwa iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita ni kuungana kwa wananchi.”
Waliotoa maoni
Kuhusu idadi ya waliotoa maoni, alisema watu wengi waliotoa maoni kuhusu Muungano walijikita katika muundo wake kama njia ya kuondoa kero,” alisema.

Alifafanua kwamba Tanzania Bara wananchi zaidi ya 39,000 walitoa maoni kuhusu muungano na kati ya hao, 27,000 walizungumzia muundo wake.
Kwa Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwenye suala la Muungano na kwamba kati ya watu 38,000 waliotoa maoni kuhusu Muungano, 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wake.
“Wananchi waliotoa maoni kuhusu muundo wa Muungano kwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 13 walipendelea Serikali moja, asilimia 24 Serikali mbili na asilimia 61 waliendekeza Serikali Tatu” alisema na kuongeza;
Utafiti wa Tume
Alisema kuwa baada ya kuchanganua sababu mbalimbali zilizotolewa na makundi mbalimbali tume hiyo ilianza kufanya utafiti wa kina kuhusu muundo wa muungano na matatizo yake tangu ulipoundwa Aprili 26, 1964, na kutaja tume zilizopendekeza Serikiali tatu.
Alizitaja tume ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka 1993, kundi la Wabunge 55 kutoka Tanzania Bara (G 55) waliopeleka bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na Tume ya Jaji Kisanga.
Changamoto Serikali Tatu
Kuhusu Serikali Tatu ambao chama tawala (CCM), kimekuwa kinaupinga kwa udi na uvumba, Jaji Warioba alisema muundo huo utakuwa na changamoto zake, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama ingawa hazitakuwa kubwa kama inavyofikiriwa.
“Gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika eneo la ulinzi na usalama, yaani jeshi la wananchi, polisi, usalama wa taifa na mambo ya nje. Gharama hizo hazibadiliki, zinabaki zile zile bila kujali kama ni muundo wa Serikali mbili au Serikali tatu,” alisema.
Alisema tangu Muungano uundwe, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimekuwa zikiongeza wizara, mikoa, wilaya na taasisi mbalimbali za kiutawala ili kuleta ufanisi na hivyo kuongeza matumizi ya Serikali.
“Tume imependekeza kodi ya bidhaa iwe ya Muungano, pia mapato yasiyo ya kodi, mikopo na michango ya nchi washirika. Ushuru wa bidhaa utakidhi sehemu kubwa ya gharama za muungano,” alisema na kuongeza:
“Kwa upande wa matatizo ya kiutendaji, tume imependekeza muundo wa Serikali tatu ujengwe kwenye misingi minne ya utendaji – muungano wa hiyari, ushirikiano, mshikamano na kutegemeana.

Thursday, January 23, 2014

JUAN MATA KAMILISHA DILI LA KUJIUNGA NA NA MAN UNITED


Club ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imekubali ofa ya paund za kiingereza £37million kutoka kwa Club pinzani ya Manchester United, kama ada ya uamisho wa kiungo mshambuliaji Juan Mata na mapema iwezekanavyo mchezaji huyu wa kimataifa wa Hispania ataruhusiwa kujiunga na Manchester United kukamilisha hilo dili hili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.



Mata atachukua vipimo siku ya Alhamisi kabla ya kukamilisha uamisho wake, ambao utamfanya kupata mara mbili ya mshahara aliokuwa anaupata chelsea kwa wiki.
Juan Mata

Wednesday, January 22, 2014

MANAIBU WAZIRI WIZARA YA FEDHA WAINGIA OFISINI LEO

Manaibu waziri wapya wa wizara ya fedha leo wamewasili katika ofisi zao tayari kuanza kazi baada ya kuapishwa na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete siku chache zilizopita. Manaibu hao Mh.Mwigulu Nchemba na Adam Malima walilakiwa na wafanyakazi wlte wa wizara ya fedha.
Mh. Mwigulu Nchemba.
Mh. Adam Malima
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha.

Thursday, January 2, 2014

WAZIRI WA FEDHA WA TANZANIA DR. MGIMWA AFARIKI DUNIA

Waziri wa Fedha wa Tanzania Dr. Mgimwa amefariki dunia jana tarehe 1 Juanuary 2014 nchini Afrika ya Kusini alipokuwa amelwazwa kwa matibabu. Mwili wa marehemu utawasili kwa ndege kutoka nchini Afrika ya Kusini siko ya Jumamosi na baadae Jumatatu kusafirishwa mkoani Iringa kwa ajili ya mazishi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.


Waziri wa Fedha Dr. Mgimwa enzi za uhai wake.

Thursday, December 12, 2013

MDAU FRANK KANANI AFUNGA NDOA NA BI. MARIA SABEGA

Mkurugenzi wa blog hii ya Njia ya Kanani Bw. Frank J. Kanani jumamosi ya tarehe 9 Novemba alifunga pingu za maisha na Bi. Maria Sabega katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Batholomayo lililopo Ubungo jijini Dar-es-Salaam na baadae katika tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Delux Sinza.

Bw. Frank J. Kanani na Bi. Harusi Maria Sabega.

Agano la ndoa.





















Friday, December 6, 2013

NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Bw. Nelson Mandela "Madiba" amefariki dunia jana katika hospitali aliyokuwa amelazwa kwa muda mrefu. Habari kutoka katika chombo kinachoaminika zinasema marehemu Mandela aliaga dunia jana na maandalizi ya mazishi yanafanywa.

Friday, November 29, 2013

UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI WAENDELEA KWA KASI

Ujenzi wa daraja kiunganishi kati ya wakazi wa Kigamboni na Kurasini umeendelea kwa kasi inayoridhisha kutokana na maendeleo yanayoonekana linde upitapo mahali hapo. Daraja hilo linatazamiwa kuzinduliwa mwaka 2015 baada ya matendenezo yake kumalizika. Picha na mdau wetu.