Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Thursday, September 15, 2016

KONA YA LIVE FOOTBALL......LIGI YA UEFA EUROPA

Manchester united leo itakuwa kibaruani wakati itakapokuwa mgeni wa timu ya Feyenoord katika mji wa Rotterdam nchini Uholanzi... Mtanange huo unategemewa kupigwa mnamo saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki

Thursday, March 24, 2016

MAKONDA, MKUU MPYA WA MKOA MWENYE HOFU YA MUNGU

Mkuu mpya wa mkoa wa Dar-es-Salaam Mh. Paul Makonda ameonesha ni kiongozi shupavu na mwenye hofu ya Mungu. Hayo yamethibitika baada ya kuonekana akipata mibaraka kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini akiwemo Kiongozi wa Wakatoliki Kadinali Pengo.

Tuesday, March 15, 2016

EPL: LEICESTER CITY YAIBANJUA NEWCASTLE UNITED NA KUJIIMARISHA KILELENI

Timu ya soka ya Leicester City imeibanjua timu ya Newcastle kwa bao moja bila na kuendelea kuongoza ligi kuu ya England.
Katika mchezo huo, mshambuliaji kutoka Japani Ozaki aliipayia timu yake bao pekee la ushindi.

Monday, March 14, 2016

PICHA 7: MBWANA SAMATTA ALIVYONG'AA UBELIGIJI

Mshambuliaji wa timu ya KRC Genk ya nchini Ubeligiji Mtanzania Ally Mbwana Samatta ameendelea kuwika mwishoni mwajuma hili baada ya kuiongoza timu yake kuibanjua timu ya Oostvede FC kwa magoli 4-1 katika dimba lao la nyumbani.
Samatta alikuwa wa kwanza kuifungia timu yake bao katika dk 23 baada ya kuunganisha kwa kichwa cha kuibia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kushoto. Mpaka sasa Samatta ameshacheza mechi 6 na amekwisha funga jumla ya mabao 2.

Akiwahadaa wazungu.....

Samatta akifunga bao kwa kichwa

Samatta akipongezwa na wenzake..

Thursday, February 11, 2016

AJALI YA BASI LA SIMBA MTOTO

Basi la Kampuni ya SIMBA MTOTO lililokuwa linatokea Tanga asubuhi hii limepata ajali maeneo ya mkanyageni kwa kugongana na lori uso kwa uso inasadikiwa watu wengi wamefariki akiwamo Dereva na Kondakta wake. Picha na ripota wetu

 
 

UZEMBE WA KIVUKONI WAHATARISHA MAISHA YA WAKAZI WA KIGAMBONI

Wakazi wa Kigamboni asubuhi ya leo wamenusurika kuzama baharini baada ya kivuko cha MV Kigamboni kujaza abiria kupita kiasi na kusababisha kivuko hicho kushindwa kuinua milango yake. Picha na ripota wetu.

Kivuko kikijaza abiria zaidi ya uwezo wake
 
Mlango wa Kivuko ukigoma kufunga 
Abiria wakijitosa baharini kuokoa maisha yao.. 

Tuesday, June 30, 2015

WALIMU WANYANYASWA KISHIRIKINA BUNDA

MBUNGE wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola amelazimika kukatisha vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma kwenda jimboni kwake, kijiji cha Nambaza, kata na tarafa ya Nansimo, wilaya ya Bunda mkoani Mara kushughulikia adha wanayoipata walimu wa shule ya msingi kijijini hapo wanaofanyiwa vitendo vya kishirikina, kudhalilishwa na kuteswa kishirikina na kulazimika kuomba uhamisho wakafundishe shule nyingine maeneo ya mbali na jimbo hilo.

Walimu wa shule hiyo ya msingi Nambaza wanadai usiku wakiwa wamelala wanaingiliwa na wachawi ambao wamekuwa wakiwanyoa nywele sehemu za siri, kuwafanyia vitendo vya ngono, kuwalawiti na kuwaibia mali na fedha kishirikina.

Aidha walimu hao wanadai kwamba, mbali na vitendo hivyo vya kuingiliwa kimwili, kulawitiwa, kunyolewa nywele sehemu za siri, kuibiwa mali na fedha kishirikina, pia wamekuwa wakikuta mikojo, ugali na samaki ukiwa umefunikwa na shuka kitandani, hali ambayo imewafanya washindwe kufundisha na kuomba wahamishwe katika shule hiyo.

Mwalimu Joyce Maugo ambaye ni mkongwe kidogo katika shule hiyo, kwa masikitiko huku akibubujikwa na machozi alisema, walimu wa shule hiyo wako hatarini kwa vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa, alisema mmoja wa walimu wenzake, msichana mdogo na mdogo kimaumbile aliingiliwa kimwili kishirikina mpaka kazimia.

Alisema, asubuhi alipoitwa kwenda kushuhudia yaliyomkuta mwalimu huyo mwenzake,  alikuta mambo ya aibu amefanyiwa mwalimu huyo, alikuwa hawezi kutembea, sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya, kitanda kikiwa kimevurugwa hovyo hovyo, kikiwa na kinyesi, damu na mikojo kibao!

Bi. Joyce alisema mwalimu wa kiume Pasco Mayamba akiwa amefunga milango na madilisha ya chumba chake, asubuhi alipoamka alikuta madirisha na milango iko wazi, kitanda kimejaa mkojo, kitandani kwake ndani ya shuka alilojifunika kukiwa na bonge la ugali, kipande cha mnofu wa sangara na mchuzi mwingi.

Alisema, wakati fulani wakila chakula usiku, ghafla chakula kinabadilika, kama ulikuwa wali na nyama unakuwa ugali na dagaa au mboga za majani hali ambayo alisema ni ya mateso, adha na manyanyaso makubwa wanayoyapata nakuomba wahurumiwe, kama kuna makosa wamewafanyia wawaambie wawaombe msamaha ili wasiendelee kuwatesa na kuwanyima raha na amani kimaisha.

Mwalimu Lucy alisema, mbali na adha hizo watu hao wanawaibia fedha, vitambulisho, kadi za benki na mali nyingine, lakini pia wakati mwingine wanakuta mkojo na kinyesi katika madebe ya unga na chungu cha mboga vitendo ambavyo vinawanyima morari ya kazi na ari ya kuendelea kufundisha shule hiyo.

Kwa sasa mwalimu Lucy alisema watu hao wanahisaidia haja kubwa madarasani na kuwapa kibarua walimu na wanafunzi kuzoa kinyesi madarasani karibia kila siku na kuwasihi viongozi na wanakijiji wa kijiji hicho waliowema kuchukuwa hatua dhidi ya madhira hayo kwa walimu.

Akizungumza na majira jana akiwa mjini Bunda, mbunge Kangi alisema vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa walimu hao ambao ni wageni,  waliopelekwa shuleni hapo hivi karibu siyo vya kufumbiwa macho, ni vya kukemewa vikali na wahusika wakibainika wachukuliwe hatua kali kwani, mbali na madhara wanayoyapata walimu hao kwa kuingiliwa kimwili bila ridhaa yao na watu wasiowajua wala kuwaona,  pia vinawadhalilisha na vinalenga kudidimiza maendeleo ya elimu katika jimbo lake.

Kangi alisema,  amelazimika kwenda kijijini Nambaza kulishughulikia tatizo hilo ambapo leo Jumatatu, Juni 29, 2015 atafanya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho ili kutafuta ufumbuzi na dawa ya tatizo hilo ili likomeshwe na lisitokee tena.

Wananchi wa kijiji hicho katika mkutano wao wa hadhara walioufanya hivi karibuni waliwabaini kwa kuwapigia kura baadhi ya wanakijiji hicho kuwa ni wahusika wakuu katika kuwafanyia vitendo hivyo vya kishirikina walimu hao, kiongozi na kinara wa mch ezo huo mchafu akitajwa mmoja wa viongozi kijijini hapo anayeishi eneo jirani na shule hiyo.

Wanakijiji wa kijiji hicho waliazimia washukiwa hao wahame haraka kijijini hapo kabla hawajachukua sheria mkononi wakidai vitendo wanavyo vifanya mbali na kuvunja sheria vitasababisha shule yao ikose walimu wa kuwafundisha watoto wao hali ambayo  inaweza kusababisha kijiji kukosa wasomi na kuwa kijiji cha wahuni na vibaka.

Kuhusu maamuzi ya wanakijiji hao ya kuwataka wakazi wenzao, wanaowatuhumu kwa ushirikina kuhama kijiji, mbunge Kangi alisema, atayaheshimu maamuzi yao na kwamba kabla wananchi hawajafikia hatua ya kuchukua sheria mkononi atawashauri watu hao wahame kijiji hicho haraka.

Mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Milumbe aliliambia majira kwamba, vitendo hivyo hawezi kuvivumilia, ni vitendo vya udhalilishaji, asivyoweza kuvifumbia macho lazima achukue hatua.

Mkuu wa wilaya Milumbe alisema, atakwenda Nambaza kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho na kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa sheria atachukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya kihuni akisisitiza ataheshimu maamuzi ya wananchi.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi. Lucy Msofe alisema,  amesikitishwa sana na vitendo hivyo wanavyofanyiwa walimu hao wenye umri mdogo na wadogo kwa maumbile akidai ni ukatili wa hali ya juu wanaofanyiwa walimu hao.

Bi. Msofe alisema, tayari amelazimika kumuhamisha mwalimu mmoja wa kike ambaye alifika kwake akiwa na hali mbaya kutokana na alivyofanyiwa na watu hao na kuongeza kwamba, endapo hali hiyo itaendelea atalazimika kuwahamisha walimu katika shule hiyo awapeleke katika shule wanayowahitaji,kuwaheshimu na kuwathamini kwani uenda shule ya msingi Nambaza hawahitajiki.

Alisema hayuko tayari kuendelea kushuhudia watoto wa watu wakiendelea kuteseka, kunyanyasika, kudhalilishwa na kufanyiwa unyama kiasi hicho akadai atawahamisha kama vitendo hivyo havitakomeshwa.

Thursday, April 9, 2015

HABARI MVUNJIKO...! AJALI MBAYA YA MABASI YATOKEA LEO

Ajali mbaya imetokea leo kati ya dasi la Ngorika na RATCO na gari ndogo na kusababisha vifo vya watu tisa na wengine wengi kujeruhiwa. Vyanzo vimedai kuwa ajali hiyo ilisababishwa na dereva wa basi la RATCO aliyekuwa akikilipita garo dogo


 
 
 
 
 

Friday, March 6, 2015

LIVE KUTOKA KATIKA MARRIAGE REVIVAL DENNER PATY

Baadhi ni matukio yanayoendelea katika dinner Party ya Marriage Revival kutoka kanisa la Mlima wa moto Mikocheni.
Washiriki wakifuatilia kwa umakini... 

Saturday, February 14, 2015

VIKOSI VYA KIGAIDI VYAJERUI ASKARI POLISI WANNE KATIKA MAPAMBANO TANGA.

Kumekuwa na mapambano yanayoendelea katika mapango ya amboni kati ya askari wa jeshi la polisi na kikundi cha kigaidi kinachosemekana kuweka kambi katika mapango hayo.
Habari zilizotufikia hivi punde zinadai kuwa katika mapambano hayo ya kivita askari wa nne wamejuruhiwa vibaya. Tutawaletea taarifa kadri zitakavyokuwa zinapatikana. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Askari akiwa katika doria.
 
Askari wakishuka katika helikopta tayari kwa mapmbano. 
 
Kituo cha Habari ITV kikitangaza mapigano hayo. 

HAPPY VALENTINE DAY

Managment ya Njia ya Kanani Blog inapenda kuwatakia wadau wote siku njema ya wapendanao duniani na kusihi tudumishe upendo na amani miongoni mwetu.

Tuesday, February 3, 2015

FAHAMU JINSI UMEME UNAOVUJA (LEAKAGE) UNAVYO KUONGEZEA GHARAMA KATIKA BILI YAKO YA UMEME

HUU NDIYO UFUMBUZI WA BILI KUBWA YA UMEME

Wengi wamekuwa wakilipa bili kubwa za umeme ambazo hata wao wanahisi sio halali ukilinganisha na matumizi yao.
Tatizo la kuvuja kwa umeme limekuwa kubwa sana,bahati mbaya mafundi wengi wamekuwa wakilitatua kwa namna ya kuliongeza badala ya kuliondoa. Tatizo hili limekuwa likitokea sana katika nyumba ambazo zinatumia vifaa vya pin tatu yaani live,neutral and earth mfano fridge,pasi,jiko la umeme, n.k.Vile vile linatokea sana katika nyumba yenye wiring iliyo choka au kwenye nyumba ambayo wire zake zimechubuka.

Kwa kawaida kuna vifaa maalumu vya kutambua uvujaji wa umeme katika nyumba kama vile EARTH LEAKAGE CIRCUIT BREAKER ingawaje nyingi zilizo fungwa majumbani siku hizi ni FEKI hivyo zinashindwa kujizima pale umeme unapo vuja.
Mara nyingi Leakage ya umeme hua inapimwa kwa kuangalia resistance between LIVE wire and EARTH wire na kiutaratibu laizima resistance ya wire hizi mbili izidi 1000000 ohms =1mega ohms Kama endapo itatokea ikwa chini ya hapo moja kwa moja tunaamini kuna gharama za ziada zitakazo ongezeka kutokana na resistance hiyo kushuka chini ya kiwango hicho. Mfano fundi umeme amepima continuity na kukuta resistance between LIVE wire and EARTH wire is 1000 ohms = 1k ohms
Mweye nyumba yenye ukinzani kama huu ataingia gharama ya ziada ambayo inasababishwa na kuvuja kwa umeme. 

HEBU TAZAMA MFANO HUU HAPA CHINI KULINGANA NA RESISTANCE HIYO HAPO JUU ITAONGEZA GHARAMA KIASI GANI KWA MTUMIAJIWA UMEME.
(i) Resistance between LIVE wire and EARTH wire = 1000 ohms
(ii) Tafuta Current (I) Current (I) =V/R
NOTE:-Umeme unaoingizwa majumbani wa single phase ni 220 Voltage.
Hivyo Current(I) =V/R = Current (I) =220/1000=0.22Ampere
(iii) Tafuta power Power (P) =Voltage(V) X Current(I) Hivyo P=VxI P=220 x 0.22= 48.4 watt
P=48.4watt.
NOTE:-Gharama za Unit moja ya tanesco ambayo ni sawa na 1000watt ni 306.52Tsh,hii ni kwa wale wanao tumia zaidi ya Unit 50Kwh.

TAZAMA JEDWALI HILI KWA UFAFANUZI ZAIDI:
Domestic Low Usage Tariff (D1)
This category covers domestic customers who on average have a consumption pattern for 50 kWh. The 50 kwh are subsidized by company are not subjected to service charge. Under the category any unit exceeding 50 kwh is charged a higher rate up to 306.52Tsh. In this tariff category, power is supplied at a low voltage, single phase (230 V).

General usage Tariff (T1)
This segment is applicable for customers who use power for general purposes: including residential, small commercial and light industrial use, public lighting, and billboards. In this category the average consumption is more 306.52Tsh. per meter reading period. Power is given at low voltage single phase (230), as well as three phase (400V).

Low voltage maximum Demand (MD) usage tariff (T2)
Applicable for general use where power is metered at 400V and average consumption is more than 7,500kWh per meter reading period and demand doesn’t exceed 500KVA per meter reading period. High Voltage Maximum Demand (MD) usage tariff (T3).
Applicable for general use where power is metered at 11KV and above.

Tariffs:
Domestic Low Usage (D1)
General Usage (T1)
Low Voltage Max (T2)
High Voltage Max (T3)

NOTE:
All the charges above exclude VAT and EWURA Au tembelea Tanesco Electricity Charges.

Kama tulivyoona 1unit it cost 306.52Tsh if your consumption is more than 50Kwh
Hivyo basi Tukitaka kujua gharama za uvujaji wa umeme kwa resistance hiyo hapo juu (gharama hii ni ya umeme unao vuja bila kujali umetumia umeme au hujatumia) ni kama ifuatavyo:-
Cost = (Consumption watt /1000) x Time x 306.52 Kwh Cost =
(48.4w/1000w) x 720 hrs x 306.52Kwh=10,681.6Tsh
Cost consumption is 10,681.6Tsh.

Hivyo kama resistance between LIVE wire and EARTH wire is 1000 ohms you have fixed added cost of 10,681.6Tsh on your normal consumption cost. Hii inamaanisha kama matumizi yako ya ndani ya halali unayotumia mfano ni ya 52000 itakubidiulipe 62681.6Tsh badala ya 52000.
NOTE:-
The added cost may either decrease or increase due to the either increase or decrease of the resistance respectively between live wire and earth wire
This means the high the resistance between the LIVE wire and the EARTH wire=low added cost and the low resistance between the LIVE wire and the EARTH wire=high added cost
IT SUGGESTED THAT THE RESISTANCE BETWEEN THE LIVE WIRE AND THE EARTH WIRE SHOULD BE MORE THAN 1000000 ohms = 1mega ohms
THIS IS APPLIED THE SAME TO THE RESISTANCE BETWEEN LIVE WIRE AND NEUTRAL WIRE DURING “off state” OF THE CIRCUIT.

Kama unahisi unalipa bili ya umeme zaidi ya matumizi yako hakikisha unawasiliana na fundi umeme aje kukupimia continuity ya wiring yako.
ZINGATIA:-Kitaalamu uvujaji wa umeme unaopelekea kuongezeka kwa bili ya umeme hakutibiwi kwa kubadilisha EARTH ROAD kama wengi wanavyo fanya,utaweza kuondoa tatizo hilo kwa ku-trace eneo linalo vujisha umeme na kuliondoa.
HAKIKISHA FUNDI WAKO ANA KIFAA CHA KUPIMIA CONTINUITY “MEGA” ILI AWEZE KUTAMBUA RESISTANCE BETWEEN THE WIRES ON YOUR CIRCUIT.
Any obtained resistance can help to determine the added cost by above formula.
PENDELEA KUKAGUA WIRING YAKO KILA BAADA YA MIEZI SITA KWA USALAMA WA UCHUMI WAKO, MALIZAKO NA UHAI WAKO.



IBRAHIM ABDALLAH MAKBEL
C.E.O FAABI ELECTRICAL AND SECURITY SYSTEM

MAWASILIANO:
+255787577755
+255767577755
+255717577755
+255777077755
FAABI TEAM TUPO KWA AJILI YENU NA MALI ZENU.
Email: faabielectrical@gmail.com

 

Monday, January 5, 2015

BREAKING NEWS!! MABASI MATANO YAPATA AJALI YAKITOKEA KILIMANJARO

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba kuna mabasi matano yamegongana njia ya kwenda Arusha toka Dar-es-Salaam asubuhi ya leo. Habari za kuaminika zinasema moja ya mabasi hayo ni Kilimanjaro Express na hadi sasa bado haijajulikana idadi ya majeruhi wala waliopotenza maisha ni wangapi. Punde itawajia habari kamili.

 
 
 
 

Friday, January 2, 2015

BREAKING NEWS!!! PANYA ROAD WAITIKISA DAR USIKU HUU

TAHARUKI YA 'PANYA ROAD': Kundi maarufu kwa jina la Panya Road lavamia maduka, lanyang'anya watu mali zao External Ubungo, Dar leo usiku. Katika taharuki hilo watu walionekana wakihamaki na kukimbia huku na kule ilimradi kila mtu ni kuepusha maisha yake! Habari zaidi bado repota wetu anazifuatilia.....

Wednesday, December 31, 2014

MTUHUMIWA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAHAKAMANI

Mtuhumiwa wa kesi ya madawa ya kulevya leo majira ya asubuhi aliuwawa kwa kupigwa risasi na askari magereza baada ya kushindwa katika jaribio la kutoka kutoroka. Mtuhumiwa huyo akiwa amefikishwa mahakamani kutoka mahabusu aliwakimbia walizi hao na kuparamia ukuta wa mahakama akiwa na lengo la kutoroka kabla ya kuuwawa na askari hao waliokuwepo mahakamani hapo. Picha zaidi na wadau wetu. Baadhi ya picha kwa hisani ya Global Publishers