Thursday, November 20, 2014
Friday, November 14, 2014
BREAKING NEWS!! MACHINGA COMPLEX YAUNGUA MOTO
Thursday, November 13, 2014
MAJIBU YA SMS KWA MPENZI WAKO VYENYE VIASHILIA VYA KUOMBWA HELA
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''
2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.
Thursday, November 6, 2014
MWANAMKE ATUPA KITOTO KICHANGA CHOONI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.
Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.
Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014