Club ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imekubali ofa ya paund za kiingereza £37million kutoka kwa Club pinzani ya Manchester United, kama ada ya uamisho wa kiungo mshambuliaji Juan Mata na mapema iwezekanavyo mchezaji huyu wa kimataifa wa Hispania ataruhusiwa kujiunga na Manchester United kukamilisha hilo dili hili katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
Mata atachukua vipimo siku ya Alhamisi kabla ya kukamilisha uamisho wake, ambao utamfanya kupata mara mbili ya mshahara aliokuwa anaupata chelsea kwa wiki.
Juan Mata