Wednesday, December 31, 2014
MTUHUMIWA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI MAHAKAMANI
Sunday, December 7, 2014
MDAU WENU NILIPOTEMBELEA MOJA YA MAAJABU 7 YA DUNIA KASRI YA TAJ MAHAL NCHINI INDIA
Thursday, November 20, 2014
Friday, November 14, 2014
BREAKING NEWS!! MACHINGA COMPLEX YAUNGUA MOTO
Thursday, November 13, 2014
MAJIBU YA SMS KWA MPENZI WAKO VYENYE VIASHILIA VYA KUOMBWA HELA
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''
2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako.
Thursday, November 6, 2014
MWANAMKE ATUPA KITOTO KICHANGA CHOONI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.
Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.
Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.
Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.
Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.
Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.
Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014
Monday, November 3, 2014
MKUTANO WA MWALIMU NYERERE FOUNDATION KUHUSU KATIBA MPYA WAFANYIWA VURUGU
Sunday, November 2, 2014
Thursday, July 24, 2014
MKE WA MTU SUMU! JAMAA APIGWA NA SULULU KATIKA FUMANIZI
Wednesday, July 2, 2014
BREAKING NEWS!!! MAJAMBAZI YAFANYA JARIBIO LA KUTOROSHA WAFUNGWA
Monday, June 30, 2014
Thursday, June 26, 2014
MBUNGE WA KIGAMBONI DR. F. ANDUNGULILE AONGEA NA TANESCO KUHUSU KERO ZA UMEME
Mrejesho wa suala la umeme kwa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kigamboni
Siku ya Jumatatu tarehe 23.06.2014 nilifanya mkutano na uongozi wa Tanesco ngazi ya Mkoa wa Temeke na Wilaya ya Kigamboni. Mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na:
Kukatika kwa mara kwa mara kwa umeme Umeme mdogo kwa baadhi ya maeneo Uunganishaji wa umeme kwa wateja wapyaMiradi mipya ya umeme kwa Jimbo la Kigamboni
1. KUKATIKA KWA MARA KWA UMEME JIMBO LA KIGAMBONI
Umeme unaopatikana kwa wateja wa Jimbo la Kigamboni unatoka sub-station ya Ilala. Umeme huu pia husambazwa kwa maeneo ya Temeke, Mbagala na Mkuranga. Kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji pamoja na uchakavu wa miundombinu, kumekuwa na ukatikaji wa umeme mara kwa mara.
Tanesco walinieleza kuwa hatua ambazo wanachukua kuondoa tatizo hili ni pamoja na maboresho ya miundombinu, kusafisha njia unaopita umeme huo kwa kukata miti na matawi na kujenga sub-station mpya maeneo ya Mbagala. Kukamilika kwa sub-station ya Mbagala utapunguza utegemezi uliopo sasa kwa sub-station ya Ilala. Kazi ya ujenzi wa sub-station mpya unatarajia kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
2. UMEME MDOGO KWA BAADHI YA MAENEO (LOW VOLTAGE)
Kuna baadhi ya maeneo kama vile Kijichi na Magogoni kumekuwa na tatizo la umeme mdogo. Tanesco walinitaarifu kuwa kuna mpango wa kufanya “voltage improvement” kwa kufanya “phase addition” na kuongeza transfoma nyingine mbili maeneo ya Magogoni. Transfoma zipo na ninatarajia kazi hii itaanza hivi karibuni. Kwa upande wa Kijichi, pamoja na “voltage improvement” bado kutakuwa na tatizo. Suluhu ya kudumu itakuwa kukamilika kwa sub-station ya Mbagala.
Tulikubaliana kuwa kazi hii iwe imekamilika ndani ya miezi mitatu ijayo.
3. UMEME KWA WATEJA WAPYA
Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi toka kwa wananchi wengi ambao wamekuwa wakisubiri muda mrefu kupata huduma ya umeme. Malalamiko yamekuwa yakitoka Kibada, Gezaulole, Toangoma, Saku, Rufu na Kiponza.
Uongozi wa Tanesco ulinihakikishia kuwa maandalizi yamekamilika kwa ajili ya usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya Kibada (blocks 14,15,16,17,18,19,20). Waliahidi kukamilisha kazi hii ifikapo mwezi Septemba 2014.
Niliwataka ndani ya wiki tatu (3) kunipa mikakati yao ya kuwapatia umeme wananchi walioomba toka maeneo ya Gezaulole, Mbwamaji, Kizani, Mwera, Kibada(blocks zilizobaki), Ponde, Goroka Kalakala, Masaki na Malela. Uongozi wa Tanesco uliahidi kufanya hivyo kwani miradi hii imeshatengewa Bajeti zake. Pia, Tanesco haina uhaba wa vifaa vya kuunganisha umeme kwa sasa.
4. MIRADI MIPYA YA UMEME JIMBO LA KIGAMBONI
Uongozi wa Tanesco ulinitaarifu kuwa maombi yangu ya kutaka Kata za Kimbiji na Pemba Mnazi kuingizwa kwenye mradi wa Umeme Vijijini (REA) yamekubaliwa na sasa kata hizi zitaanza kupata huduma ya umeme.
Kama nilivyoeleza hapo juu, umeme wa sasa kwa Jimbo la Kigamboni hutoka Ilala, ujenzi wa Sub-Station ya Mbagala unaendelea na unatarajia kukamilika mwezi Disemba, 2014. Kukamilika kwa kituo kutafanya baadhi ya maeneo ya Jimbo la Kigamboni kujitegemea kwa huduma ya umeme na pia kuondokana kukatika katika mara kwa mara kwa umeme kama ilivyo sasa.
Vile vile Tanesco ipo kwenye mchakato wa kutafuta eneo katika Tarafa ya Kigamboni kwa ajili ya ujenzi wa sub-station mpya. Katika mwaka huu wa fedha hakuna fedha iliyotengwa kwa mradi huu. Lengo ni kuingiza ujenzi wa sub-station kwenye bajeti ijayo.
Aidha, niliwataka uongozi wa Tanesco kufanya maandalizi ya awali kujua gharama za kufikisha umeme katika maeneo ya Mwasonga, kata ya Kisarawe II ili makisio haya yaingizwe bajeti ya mwakani.Tulikubaliana zoezi hili kufanyika ndani ya miezi mitatu.
5. HITIMISHO
Shirika la Tanesco halina uhaba wa vifaa kwa sasa. Niliwataka Tanesco Kigamboni kuandaa mpango kazi wa usambazaji wa huduma ya umeme kwa wateja wapya ambayo itanisaidia kufuatilia utendaji kazi wao; kuboresha mawasiliano na mahusiano na wateja pindi umeme unapokatika au pale wateja wanapofika kuuliza kuhusu hatma ya maombi yao. Kwa vile, Tanesco ina uhaba wa vikosi vya kuunganisha umeme kwa wananchi, niliwashauri waangalie uwezekano wa kutumia wakandarasi binafsi (outsourcing) baadhi ya kazi hizi.
Kwa wananchi wa Kibada, Toangoma na Gezaulole kwa maeneo mliyoniletea orodha zenu, ndani ya siku 21 nitawapatia majibu ya lini maeneo yanatarajiwa kufikiwa. Aidha, nashauri maeneo husika kuunda kamati ambazo zinashirikiana nami katika ufuatiliaji.
Nawasilisha
Dkt Faustine Ndugulile (MB)
Mbunge Kigamboni
Friday, June 20, 2014
UINGEREZA YAPIGISHWA KWATA NA URUGUAY
Suarez alikua muiba mchungu kwa Uingereza baada ya kufunga mabao yote mawili na hivyo kuizamisha kwa mabao 2-1.