Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Tuesday, October 8, 2013

BREAKING NEWS!!!! MGOMO WA MABASI KITUO CHA UBUNGO LEO.

Mabasi yanayofanya safari za mikoani kuanzia kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar-es-Salaam leo yalifanya mgomo wa takribani masaa manne kabla ya kuanza safari  kutokana na kile walichodai Serikali kupunguza kipimo uzito wa magari katika mizani inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi kama njia ya kuepukana na uharibifu wa barabara.

Chama cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia punguzo hilo la uzito wa kipimo cha magari ya endayo mikoani kwani kipimo cha awali kilikuwa kikifikiwa kutokana na mizigo ya abilia iliyokuwa ikisafirishwa ambayo ndiyo yenye faida. Mgomo huu wa leo ulianza kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi mida ya saa mbili na nusu asubuhi mabasi hayo yalipoanza safari. Habari na Mdau wetu Frank J. Lyimo.

Abiria wanaoenda mikoani wakiwa katika sintofahamu ya hatma ya safari zao