Mkurugenzi wa blog hii ya Njia ya Kanani Bw. Frank J. Kanani jumamosi ya tarehe 9 Novemba alifunga pingu za maisha na Bi. Maria Sabega katika Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Batholomayo lililopo Ubungo jijini Dar-es-Salaam na baadae katika tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Delux Sinza.
Thursday, December 12, 2013
Friday, December 6, 2013
NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA
Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Bw. Nelson Mandela "Madiba" amefariki dunia jana katika hospitali aliyokuwa amelazwa kwa muda mrefu. Habari kutoka katika chombo kinachoaminika zinasema marehemu Mandela aliaga dunia jana na maandalizi ya mazishi yanafanywa.
Friday, November 29, 2013
UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI WAENDELEA KWA KASI
Ujenzi wa daraja kiunganishi kati ya wakazi wa Kigamboni na Kurasini umeendelea kwa kasi inayoridhisha kutokana na maendeleo yanayoonekana linde upitapo mahali hapo. Daraja hilo linatazamiwa kuzinduliwa mwaka 2015 baada ya matendenezo yake kumalizika. Picha na mdau wetu.
Tuesday, October 8, 2013
BREAKING NEWS!!!! MGOMO WA MABASI KITUO CHA UBUNGO LEO.
Mabasi yanayofanya safari za mikoani kuanzia kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar-es-Salaam leo yalifanya mgomo wa takribani masaa manne kabla ya kuanza safari kutokana na kile walichodai Serikali kupunguza kipimo uzito wa magari katika mizani inayosimamiwa na Wizara ya Ujenzi kama njia ya kuepukana na uharibifu wa barabara.
Chama cha wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani wamelalamikia punguzo hilo la uzito wa kipimo cha magari ya endayo mikoani kwani kipimo cha awali kilikuwa kikifikiwa kutokana na mizigo ya abilia iliyokuwa ikisafirishwa ambayo ndiyo yenye faida. Mgomo huu wa leo ulianza kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi mida ya saa mbili na nusu asubuhi mabasi hayo yalipoanza safari. Habari na Mdau wetu Frank J. Lyimo.
Abiria wanaoenda mikoani wakiwa katika sintofahamu ya hatma ya safari zao
Monday, September 23, 2013
TUKIO LA KINYAMA WASTGATE MALL NAIROBI TUJIFUNZE.
Shambulio la kigaidi linaloendelea kwa siku ya pili mfululizo katika eneo la biashara la Wastegate mjini Nairobi nchini Kenya inabidi liwe fundisho kwa nchi zote za Afrika kuweka maeneo ya ukaguzi wa silaha kabla ya kuingia katika eneo lolote lenye mkusanyiko wa watu wengi kama maeneo ya biashara (Shopping Malls), Viwanja vya Michezo, Maeneo ya ibada na hata katika viwanja vya maonesho na tafrija kubwa za kitaifa.
Hili litazuia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya kigaidi yanayofanya kwa malengo ya kupoteza uhai wa watu. Kitendo hiki kilichotokea Nairobi nchini kenya ni cha kinyama na kinalaaniwa na wote waliotekeleza uchama huo tunaamini watatiwa mbaroni na sheria kufata mkondo wake. Kwa pamoja tunasema poleni sana ndugu zetu wakenya mliopatwa na janga hili na Mungu awalinde.
Wasgate Shopping Mall kama inavyoonekana
Askali wakipapanda na magaidi
Wahanga wa ugaidi
Mwili wa raia aliyeuawa na magaidi
Mateka wa ugaidi
Raia akijiokoa
Monday, July 8, 2013
Subscribe to:
Posts (Atom)