Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Thursday, November 20, 2014

AJALI YAFUNGA BARABARA MIKUMI

Leo ama una safari ya kwenda Iringa, Mbeya au kama unapokwenda utapita mikumi basi sitisha safari kwani njia imefungwa tangu saa mbili asubuhi. Kuna lory linawaka moto mpaka sasa. Lilikuwa limebeba lami so lami bado inawaka na imesambaa sehemu kubwa.

Friday, November 14, 2014

BREAKING NEWS!! MACHINGA COMPLEX YAUNGUA MOTO

Soko kubwa na la kisasa lililopo maenea ya Ilala karibu na uwanja wa mpira wa Karume maarufu kama Machinga Complex linalomolikiwa na Manispaa ya Jiji la Ilala katika Mkoa wa Dar-es-Salaam, leo limeteketea vibaya na moto ulioanzia katika ghorofa ya pili. Mpaka tunapata habari hii chanzo cha moto huo kilikuwa hakijajulikana.

Thursday, November 13, 2014

MAJIBU YA SMS KWA MPENZI WAKO VYENYE VIASHILIA VYA KUOMBWA HELA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO: 
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako. ��������

Thursday, November 6, 2014

MWANAMKE ATUPA KITOTO KICHANGA CHOONI

IRINGA,
Mama mmoja mjini Iringa aamua kumtupa mtoto wake chooni mara baada ya kumzaa nyumbani.
Mtoto huyo wa kiume aliezaliwa tarehe 4/11/2014 majira ya jioni na mama huyo na kuamua kumdumbukiza chooni ambapo kisa mpaka sasa anamkwepa mumewe aliyepo safarin asijue kuwa amepata mimba na kuzaa.
Hata hivyo chanzo cha habari kinasema kuwa, mama huyo kwa jina la magdalena limano (32) mkazi wa Iringa anatabia ya kumdanganya mumewe na kutoka na mabwana wengine pindi mumewe akiwa safarini kikazi.
Mtoto huyo aliyetupwa choon majira ya jioni mara baada ya kuzaliwa na kukutwa asubuhi ya tarehe 5/11 asubuhi akiwa analia ndani ya choo na majirani na kutoa taarifa.
Mpaka sasa mtoto ni mzima wa afya na yupo katika uangalizi mzuri wa hospitali huku mama akishikiliwa na jeshi la polisi akisubiri kupandishwa mahakamani.
Picha zifuatayo linaonyesha tukio kamili: Habari kwa hisani za mtandao wa kijamii Whatsapp.

 
 Kichanga kikisafishwa mara baada ya kuopolewa chooni...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Vianney Mongella ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.

Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014

Monday, November 3, 2014

MKUTANO WA MWALIMU NYERERE FOUNDATION KUHUSU KATIBA MPYA WAFANYIWA VURUGU

Taarifa ya tukio lililotokea ubungo plaza katika mkutano wa mwalimu Nyerere foundation: Mkutano ulifanyika kuanzia saa 1520hrs ukiwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu mh. Joseph Sinde Warioba. Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na ITV na maudhui yake kimtazamo ulilenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Mh. Sitta na tume yake. Baada ya Mh. Warioba kuelezea kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ndipo wakereketwa wa upande wa Mh. Sitta walipoinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya katiba ya Mh. Sitta ambayo wao wameshaikubali? Baada ya mabango yale kuinuliwa yakazua tafrani ambapo walishauriwa kutoyainua kwa sababu haukuwa mkutano wa kisiasa na wakanyang'anywa na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti. Katika tafrani hiyo mh. Warioba alipigwa kibao na Mh. Paulo Makonda- ambaye ni katibu wa UVCCM TAIFA. Mtuhumiwa huyu pamoja na wengine wanne wamekamatwa kwa mahojiano. Upelelezi unaendelea na juhudi za kuwapata wengine zinaendelea.

Sunday, November 2, 2014

SALAMU KUTOKA INDIA

Mdau wenu yupo matembezoni nchini India na ameamua kuleta kwa kifupi mambo anayokutana nayo kwa Muda wote atakaokuwepo nchini humo. Kaa tayari kupata yatakayojili.