Advert


java

Connectify - Turn Your PC into a Wi-Fi Hotspot. Install now!

Friday, February 25, 2011

Dubaiii......

SERENGETI LAUNCHES TUSKER MALT
Minister of Industry and Trade Dr. Cylil Chami during the Launching ceremony
 
 Minister of Industry and Trade Dr. Cylil Chami (Centre), Permanent Secretary Mrs. Joyce Mapunjo (2nd left) and Serengeti Breweries Management having a toast. 

Managing Director Mr. Richard Wells of SBL during the ceremony.

Marketing Director Mrs. Caroline Ndungu of SBL during the ceremony

 

Thursday, February 24, 2011

Ligi ya Mabingwa Ulaya.....

 GOMES AIUA INTER DAKIKA YA 90





Gomes wa Beyern Munich akishangilia na Arjen Ruben baada ya kuifunga Inter Milan 1-0

GONGOLAMBOTO....

RAIS KIKWETE AZUNGUMZIA KUHUSU MAAFA YA GONGO LA MBOTO


Ndugu Wananchi,

Kama mjuavyo, jana usiku jiji la Dar es Salaam lilipata mtikisiko mkubwa kutokana na milipuko ya mabomu iliyokuwa inatokea katika ghala kuu la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lililoko Gongolamboto katika viunga vya Dar es Salaam.

Milipuko hiyo imesababisha maghala 23 kuteketea kabisa na majengo kadhaa ya shughuli mbalimbali hapo kikosini kuharibika kwa viwango mbalimbali. Mabweni mawili ya kuishi wanajeshi nayo yaliteketea. Aidha, risasi nyingi, mabomu mengi, silaha na magari kadhaa nayo yameharibiwa na mengine kuteketea. Jeshi letu na nchi yetu imepata hasara kubwa sana.

Katika maafa haya makubwa kwa taifa letu, raia nao wameathirika kwa namna mbalimbali. Nyumba kadhaa za kuishi na majengo ya huduma za jamii nayo yameharibiwa na mabomu yaliyoangukia humo. Zipo ambazo zimeungua kabisa na zipo zilizopata uharibifu mkubwa na zipo zilizopata uharibifu wa viwango vya chini.

Lakini baya zaidi, katika mlipuko huo, ndugu zetu 20 wamepoteza maisha na wengine zaidi wamejeruhiwa kwa aina na viwango mbalimbali. Baadhi yao walifika katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili na kupatiwa matibabu. Wengine wameruhusiwa na wengine wapatao 135 bado wamelazwa. Idadi kamili hupanda na kushuka kutegemea na kupokelewa na kuruhusiwa kwa majeruhi.

Ndugu Wananchi,

Hakika taifa limepata hasara kubwa kwa ndugu zetu kufariki na kujeruhiwa. Napenda kutumia nafasi hii kwa uchungu mkubwa kuelezea masikitiko yangu na taifa kwa ndugu zetu waliopoteza maisha wakati ambapo taifa lilikuwa bado linauhitaji sana mchango wao.

Naomba ndugu wa marehemu wapokee mkono wa rambirambi kutoka kwangu na kupitia kwangu kutoka kwa Watanzania wenzetu wote. Tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu marehemu wetu wapate mapumziko mema. Amin.

Aidha, kwa niaba yangu na ya Watanzania wenzangu wote, nawapa pole nyingi ndugu zetu wote waliojeruhiwa na kupata mshituko kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea jana usiku. Tunazidi kuwaombea wapone upesi ili waendelee na kazi zao za kujenga taifa pamoja na kujiletea maendeleo yao binafsi.

Leo asubuhi na baadae mchana nilitembelea eneo la tukio kule Gongolamboto na kuwatembelea wagonjwa katika hospitali za Amana, Temeke na Muhimbili. Nimeona madhara na hasara tuliyoipata pale Gongolamboto. Nimewaona na kuwafariji wagonjwa wetu. Nimezungumza na madaktari na wauguzi katika hospitali hizo. Nimewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya usiku kucha ya kuwahudumia na kuokoa maisha ya ndugu zetu hao. Nimewatia moyo na kuwataka waendelee kuwahudumia vyema.

Ndugu Wananchi,

Napenda pia kutumia nafasi hii kuwapongeza viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wa Bohari Kuu ya Madawa kwa kuhakikisha kuwa dawa na vifaa vya tiba vinapatikana kwa urahisi na kwa wakati, Hali hiyo ndiyo iliyosaidia kuokoa maisha na kuwapunguzia machugu ndugu zetu waliojeruhiwa.

Baraza la Usalama

Ndugu Wananchi,

Leo alasiri mpaka usiku huu, tulikuwa na mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Taifa. Hiki ndicho chombo cha juu cha kumshauri Rais kuhusu masuala yahusuyo usalama wa taifa letu. Kwa uzito na unyeti wa tukio, niliamua kuitisha mkutano wa Baraza hilo mara baada ya maafa hayo kutokea.

Katika mkutano wetu, tumelitafakari kwa kina tukio hili na mambo mbalimbali yanayotokana na kuhusiana nalo. Baraza limeazimia kama ifuatavyo:

1. Tumesikitishwa sana na tukio hili na hasa vifo vilivyotokea na majeraha yaliyowapata ndugu zetu wengi. Baraza limetoa rambirambi kwa ndugu na jamaa wa marehemu. Aidha, tunawapa pole wale wote waliojeruhiwa na kuwaombea kwa Mola wapone upesi.
 
2. Kuhusu waliopoteza maisha, tumeamua kuwa, Serikali igharamie mazishi ya marehemu wetu hao popote ndugu watakapoamua wakazikwe. Baadae ndugu wa marehemu wapewe kifuta machozi.

3. Kuhusu waliojeruhiwa tumeamua kuwa Serikali igharamie matibabu yao. Baadae watakapotoka hospitali walipwe kifuta machozi kwa ulemavu walioupata.

4. Kamati ya Maafa ya Mkoa imeagizwa kushirikiana na Kitengo cha Maafa cha Taifa kilichopo Ofisi ya Waziri Mkuu kuwahudumia wananchi waliopoteza makazi yao au waliolazimika kuyakimbia makazi yao kwa nia ya kuokoa maisha yao. Ihakikishwe kuwa kwa haraka wanapatiwa makazi ya muda pamoja na huduma za malazi, chakula, maji, afya na usafi wa mazingira.

5. Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa imeelekezwa kutengeneza taratibu nzuri zitakazohakikisha kuwa mapema iwezekanavyo, wananchi hao wanarejea makwao ili waendelee na shughuli zao za kawaida hasa sasa ambapo hatari ya milipuko katika maghala ya Gongolamboto haipo tena.

6. Baraza la Usalama limelipongeza Jeshi la Ulinzi kwa uamuzi wake wa haraka wa kuwatuma wahandisi wa medani kufanya kazi ya kutafuta, kutambua na kuyakusanya mabomu yote yaliyoangukia katika maeneo ya raia kwa nia ya baadae kuyaharibu.

7. Tunawaomba wananchi watoe ushirikiano wa hali ya juu kwa Jeshi kwa kuwapa taarifa wanapoyaona mabomu katika maeneo yo yote. Na, jambo kubwa zaidi tunawakumbusha wananchi kutii maelekezo ya Jeshi ya kutokuyagusa au kuchezea mabomu au hata vipande vipande vya mabomu vilivyodondoka katika maeneo yao.

8. Baraza la Usalama la Taifa, limeagiza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Maafa cha Taifa wazitambue mapema iwezekanavyo nyumba zilizoharibiwa, wenye nyumba na kuhakikisha kuwa matayarisho husika yanafanyika ikiwa ni pamoja na uthamini ili walipwe fidia wanayostahili bila kuchelewa.

9. Vile vile Kamati ya Maafa ya Mkoa imeagizwa kufanya yafuatayo:

(a) Kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwatafuta watoto waliopotea na kuwaunganisha na familia zao.

(b) Kuongoza, kuratibu na kusimamia utekelezaji wa masuala yote yahusuyo waliofariki, waliojeruhiwa na waliohama makazi yao, na huduma zao stahiki.

10. Baraza la Usalama limetoa pole nyingi kwa Mkuu wa Majeshi, Maafisa na Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa maafa makubwa yaliyowakuta na hasara waliyoipata kwa milipuko ya mabomu iliyotokea katika Ghala Kuu la Jeshi, Gongolamboto.

11. Baraza pia limelipongeza Jeshi kwa juhudi kubwa ilizofanya kuzima moto huo, hivyo kuweza kunusuru baadhi ya maghala, zana na vifaa vingine visiteketezwe na moto.

12. Baraza limeagiza Jeshi lifanye uchunguzi wake wa ndani wa chanzo cha tukio hili kama Sheria ya Ulinzi wa Taifa inavyoagiza. Aidha, imetaka vyombo vingine vya ulinzi na usalama visaidie katika uchunguzi huo.
 
13. Baraza la Usalama limeamua kuwa, Serikali ya Tanzania iombe nchi rafiki zisaidie katika uchunguzi wa chanzo cha tukio hili na kushauri namna bora zaidi ya kuimarisha usalama na uhifadhi wa mabomu na risasi katika maghala ya Jeshi letu kote nchini.

14. Mwisho, Baraza la Usalama wa Taifa linawaomba wananchi waliohama warejee kwenye makazo yao kwani kipindi cha hatari ya mabomu kulipuka kimekwishapita. Tunaomba na kusisitiza wajiepushe kuchezea mabomu yaliyodondoka katika maeneo yao ambayo bado hayajaondolewa.

 
Ndugu Wananchi Wenzangu;

Hili ni janga ambalo pamoja na kusikitisha linaleta uchungu hasa pale inapotokea miaka miwili tu baada ya janga la Mbagala. Machungu yenu ndiyo machungu yangu na ndiyo ya viongozi wote Wakuu wa Nchi yetu ambao ndiyo Wajumbe wa Baraza la Usalama la Taifa. Naomba tuwe watulivu katika wakati huu mgumu.

Napenda kuwahakikishia kuwa tumeamua kulishughulikia tatizo lenyewe na athari zake sasa na siku za usoni kwa uthabiti mkubwa. Naomba tuendelee kuwa na imani na Jeshi letu, viongozi wake na wanajeshi wetu wote. Tuwaunge mkono na kuwapa ushirikiano sasa na siku za usoni.

Mungu Ibariki Afrika!

Mungu Ibariki Tanzania!

Asanteni kwa kunisikiliza.

Monday, February 21, 2011

KWELI TEMBEA UONE....

KIBIBI CHAJIUZA MITAANI
Wadau katika pitapita mitaani nilikutana na mama mtu mzima akifanya uchangudoa mitaani mchana kweupee bila hata ya kuwa na aibu!

Mtu mzima huyo anakata mitaa akiwa na Fegi mdomoni na Kiroba mkononi




 Kikielekea dukani kuongeza kiroba na sigara





Baada ya kuambiwa lile ni duka la vifaa akaamua kununua kwenye kioksi na hapa anaomba moto



Alipoona watu wanamjalia akaamua ajikate huku akitingisha vikalio vyake!







DUNIA KWELI IMEISHA.....

NABII FEKI TITO AJA NA VITUKO VYA POMBE DAWA

Jina la Nabii Titto sio geni miongoni mwa wakazi wa jiji la Dar. Yeye anahubiri matumizi ya pombe kwa kutumia Biblia,anasema kuwa mungu ameruhusu watu wanywe pombe kwani ni tiba sahihi kwa magonjwa mbalimbali. Wadau kama sio uchizi huu ni nini?


 Nabii Tito akishika pombe na kitabu cha dini.


Juma Chikoka (Chopa mchopanga) akiwa na Jackline Wolper na Johari wakimsikiliza Nabii Titto kwa umakini mkubwa





             Kipeperushi hiki cha Nabii Titto kiliniacha hoi

Sikuamini maneno yake akatumwa mtu alete pombe na Nabii Titto bila hiyana kudhihirisha umma akakata safari beer,Wadau mpooo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj-996yXzHY5N6iGLn6lEk0uR9DtPmxdXkJVjbfRdRo0riRniO9WUVWBaszmQhCGi7f-pFckMGodam6iv9OwZXjm4sOJEZ_mu1ooP8Ar9rWq9g5h9HkG_CWq4FjP-Ke8B0DuUx284z6LVU/s400/DSC02444.JPG
 

    Nabii Titto akinukuu neno kutoka kwenye kitabu cha      mungu(BIBLIA)kinachoruhusu matumizi ya pombe huku pombe yake ikiwa pembeni.



Wednesday, February 16, 2011

VILIO VYATAWALA GONGOLAMBOTO

MABOMU YALIPUKA GONGOLAMBOTO JANA USIKU



Usiku huu hali shwari katika maeneo ya Gongolamboto, kisarawe na jiji zima la Dar-es-Salaam Kiujumla kutokana na mabomu yanayolipuka kwa kasi kutoka katika kambi mojawapo ya JWTZ iliyipo katika maeneo hayo!

Msemaji wa JWTZ amesema haijulikani mabomu hayo yataisha saa ngapi. Wakazi wa maeneo hayo na ya karibu wanashauliwa kukimbilia maeneo ya katikati ya mji ili kujinusuru na mhanga huu.

Habari zisizo rasmi zinadai kuwa mali nyingi na nyumba zinaendelea kuharibika kutokana na milipuko hii inayoendelea. Habari zaidi kama zinavyoonekana katika picha.



Picha inayoonyesha mwanga mlipuko angani.
Baadhi ya wahanga wa mabomu wakikimbizwa hospital.



Wakazi wa Gongolamboto wakikimbia kutoka majumbani kwao.

Miale mikubwa ya moto ikionekana toka pande zote za jiji la Dar-es-Salaam 

  
Moja kati ya nyumba zilizotuliwa na mabomu.

Kombola likiwa limetua kwenye moja ya kuta.




Wakazi wa Kimara wakiangalia mabomu yaliyotua katika maeneo yao.

Tuesday, February 15, 2011

NAULI MIKOANI KUWA JUU

 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Maji na Nchi Kavu Nchini, (Sumatra), imeridhia kupandishwa bei za nauli mpya za mabasi yaendayo mikoani kuanzia Jumanne ijayo.

Uamuzi uliotolewa na Bodi ya Mamlaka hiyo baada ya kusikiliza maombi ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Nchini (Taboa), yaliyofikishwa kati ya Desemba nane na 17, mwaka huu umeridhia kuwa nauli kwa mabasi ya kawaida kupanda kutoka Sh 26. 6 kwa kilometa hadi Sh32.20.

MBOWE ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI KIVULI BUNGENI


KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe jana alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli likiwa na mawaziri 29 wote kutoka Chadema.

Katika Baraza hilo, Mbowe amewateua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa Waziri Kivuli wa Fedha, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kwa mujibu wa Mbowe, Waziri Kivuli katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), amekuwa Raya Ibrahim Khamis, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji amekuwa Esther Matiko huku naibu wake akiwa Vicent Nyerere.

Mbowe alimteua Said Amour Arfi kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mchungaji Israel Natse kuwa Waziri wa Mahusiano na Uratibu, huku Susan Lyimo akiteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Leticia Nyerere Waziri wa Ofisi hiyo akishughulikia mazingira ambapo Zitto Kabwe amekuwa Waziri wa Fedha huku naibu wake akiwa Christina Mughwai.

Godbless Lema amekuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Tundu Lissu, Katiba na Sheria, Ezekia Wenje akienda Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Joseph Selasini alipewa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Silvester Kasulumbai akiteuliwa kuongoza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine walioteuliwa na wizara zao katika mabano ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Halima Mdee (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Mchungaji Peter Msigwa (Maliasili na Utalii).

Mhandisi Salvatory Machemuli ataongoza Wizara ya Ujenzi, Mhonga Ruhwanya (Wizara ya Uchukuzi), Lucy Owenya (Viwanda na Biashara), Christowaja Mtinda (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Dk Gervas Mbasa (Afya na Ustawi wa Jamii).

Pia wamo Regia Mtema (Kazi na Ajira), Naomi Kaihula (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Joseph Mbilinyi (Habari,Vijana na Michezo), Mustapha Akunaay (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Meshack Opulukwa (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Highness Kiwia amekuwa Waziri Kivuli wa Maji. 

Monday, February 14, 2011

HAPPY VALENTINE!!!!








Napenda kuwatakia sikukuuu njema wadau wote wa Njia ya Kanani katika siku ya hii ya kuonyesha upendo kwa wale tuwapendao ila sio lazima kuwapenda wote! Don't pretend! Kama humpendi vilevile muoneshe kwamba humpendi



Thursday, February 10, 2011

SONGOMBINGO LA KUFUMANIWA

Mume aingiza hawara ndani ya nyumba yake, na kulala naye mpaka asubuhi. Mke alala chumba cha watoto, mfumaniwaje ajieleza 'live' bila chenga!

LEO TENA CHA CLOUDS NA BETHIDEI YA MIAKA 7


Kipindi cha Clouds FM cha leo tena kinatimiza miaka saba.

Tuesday, February 8, 2011

NJIA YA KUPUNGUZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

By Mdau.


Tunapozungumzia upungufu wa nguvu za kiume tunakuwa katika uwanja mpana zaidi wa tafakari za kibaiolojia na kisaikolojia walizonazo wanaume. Lakini kwa kufupisha mlolongo wa mambo sehemu kuu tatu zinaweza kabisa kukidhi mchanganuo mzima wa jinsi tatizo hili linavyowasumbua wanaume wengi duniani.
Sehemu kubwa ya malalamiko ya wanaume katika sakata hili yanagusa zaidi maeneo matatu ambayo ni KUKOSA MSISIMKO, KUSHINDWA KURUDIA TENDO NA KUKOSA KABISA NGUVU, huku kufika kileleni mapema kukihusishwa pia kama pacha wa janga hili ambalo linawasumbua zaidi wanaume, ingawa na wanawake wanakabiliwa na sehemu ndogo ya tatizo hili.
Hata hivyo uchunguzi wa hivi karibuni uliowahusisha wanaume wanaofika kliniki au kupata tiba za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume umeonesha kuwa, sio wanaume wengi wenye sababu za kibaiolojia zinazowafanya wakose nguvu za kiume, isipokuwa wengi wao huwa na matatizo ya kisaikolojia zaidi ambayo wahusika wanaweza kujiponya nayo bila hata kutumia vidonge wala dawa za miti shamba.

Ingawa Matabibu wanataja magonjwa ya moyo, kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya zinaa, unene wa kupita kiasi, umri mkubwa kuwa ndiyo chanzo cha wanaume kupungukiwa na nguvu za kiume, lakini imebainika kuwa idadi kubwa ya wanaume wanaofika hospitalini kutafuta nguvu za kiume hawana magonjwa hayo
Huu ni ushahidi kuwa wanaokabiliwa na janga hili wamebeba tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kimawazo zaidi kuliko hali halisi. Ukweli wa mambo ulioibuliwa na wanasaikolojia umebaini kuwa, wale wote wanaolalamikia/lalamikiwa kuwa hawana nguvu iwe ya kufika kileleni mapema, kutokuwa na msisimko na kushindwa kurudia tendo wamekosa maarifa tu ya kufahamu na hawaijui miili yao na kwamba wanaishi kwa kusikia zaidi ya kujitambua.

Katika hali ya kawaida kila mwanadamu ameumbwa kwa njinsi yake na inapotokea kushabihiana basi ni bahati, lakini mara nyingi usawa hupatikana kwa mmoja kujifunza au kusaidiwa kufikia kiwango cha mtu anayemuhitaji kuwa nae katika maisha hasa ya kimapenzi. Jambo hili wataalamu wanasema kuwa miili iko tayari kutii mafunzo na kubadilisha tabia zake kulingana na utashi wa mhusika.
Tatizo kubwa lililopo kwa wapenzi wengi wanaolalamikia upungufu wa nguvu ni kwamba maisha yao wanayachezea kwenye viwanja vya wenzao wanaokutana nao katika vijiwe na sehemu za kazi. Usikivu wa mazungumzo toka kwa wanaume wengine wenye uwezo wa kwenda mara nne hadi saba katika tendo au wanatumia dakika arobaini kufika kileleni umewafanya wanaume wengi kujihisi tu kuwa wao wanakasoro eti kwa kuwa huishia mara mbili au moja katika kufanya tendo.
Dhana ya kujiona ni mwenye kasoro inapojengeka akilini mwa mwanaume, huchipua hofu na hatimaye kumfanya ashindwe kabisa kusisimka anapofikiria au kukutana na mwanamke. Matokeo ya hangaiko la akili hushusha uwezo wa mwili na kumuongoza mtu kwenye kuwaza ugonjwa kisha kukimbilia hospitali au kwa waganga kutafuta tiba ya ugongwa ambao kimsingi hanao.

Lakini ukweli uko wazi kwamba kukimbilia kutafuta uwezo wa kufanya mapenzi mara sita au saba hakumfanyi mwanaume awe mlinganifu mwenye kusifiwa na wanawake wengi, kwani si wanawake wote wana uwezo wa kufanya mapezi kwa raundi hizo na si wote wanapenda kutumia takika 30 kucheza mpira wa kikubwa, wengine hukinai mapema na huona kero kuwa na wanaume ving’ang’anizi wenye sifa za kuganda wanapopewa.

Kwa kufahamu haya utagundua kuwa kukimbilia kutafuta tiba ya kumudu kwenda mara saba ni jitihada mfu kabisa zisizohitajika katika maisha ya mwanaume hasa ukizingatia kwamba wenye uwezo wa kufanya mapenzi mara nyingi hawakuzaliwa hivyo, bali walijizoeza kupitia mazingira ya malezi na makuzi yao. Maana hawezi kuwa mzoefu wa raundi mvulana aliyelelewa katika mafundisho ya kukatazwa ngono na kulindwa hadi akakakua.
Kadhalika hawi hodari wa kimapenzi msichana aliyefundishwa kujitunza, yote yatakayofuata kwa mvulana au msichana humea baada ya kupandwa na tabia chipukizi za ukubwani. Kwa msingi huo mwanaume anajukumu la kuutengeneza mwili wake uwe katika staili aitakayo. Ndiyo maana kuna wengine hawamudu kulala bila kufanya ngono, hii ikiwa na maana kuwa wamejizoeza tu, si kwamba wameumbwa na nguvu hizo.
Labda ili kufikia kilele cha somo hili ni vema tukalejea matatizo matatu niliyosema hapo juu ili tujue ni jinsi gani tunaweza kuepukana nayo bila hata kumeza vidonge na tukawa wanaume wa mbegu kama wengi wenu mjuavyo. Kwa kuanza tuzungumzie Kukosa msisimko. Hapa tunatakiwa kuajitambua sisi wenyewe kwanza, tukijua historia na mazingira yetu ya kimapenzi.
Kwa wanaume ambao wamebanwa sana kikazi na hufanya mapenzi mara moja moja, hukabiliwa na tatizo la kukosa msisimko kwa sababu miili yao imezoea. Sasa ili kuifanya ichangamke lazima waanze kuirejesha kwa kufanya mapenzi mara kwa mara na kwa raundi chache. Kisha wanatakiwa kufanya mazoezi na kula vyakula, vinywaji vyenye nguvu ili kujipa nguvu.

Pia kama mwanaume ameishi na mwanawake kwa muda mrefu na amekuwa na desturi ya kufanya mepenzi mara kwa mara katika mazingira yale yale anaweza kukumbwa na kasoro hiyo. Hivyo anashauriwa kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi, kupeana mahaba mapya, kuamsha mapenzi kwa kujaliana, pia kuondoa fikra zote zenye kukinaisha ikiwa sambamba na kuzingatia usafi wa mwili. Yakifanyika hayo mwili utaitikia taarifa ya akili na nguvu zitapatikana.

Kwa wanaoshindwa kurudia tendo wanatakiwa kufuata kanuni hizo hapo juu. Jambo kubwa ni suala la kuuzoeza mwili. Usiulazimishe kuanza mara moja kwenda mara nyingi wakati mapenzi yako yamekuwa ya kuiba mpaka baba alale na wakati mwingine muda wako wa kutoka kazini umebana na hivyo kukufanya ufanye mapenzi ya chap chap kila siku. Ukiwa mtu wa namna hii haiwezi ikatoke siku moja ghafla tu ukafanya mpenzi mara tatu bila kuchoka.
Pia inawezekana mwanaume akashindwa kurudia tendo si kwa sababu hana nguvu bali hapewi ushirikiano wa kutosha toka kwa mpenzi wake. Hivyo wakati wa kutafuta uwezo wa kwenda raundi nyingi ni vema usaidizi wa mwanamke ukatolewa, isitokee kupokea lawama tu za “huwezi, sijatosheka” kwani hizo ndizo zinazowafanya wanaume washindwe kabisa kwa hofu kuwa wanaaibika. Mawazo ya kuaibika yanapopewa kipaumbele huufanya uume kuzidi kusinyaa, kwa maana hiyo ni vema kuyatupilia mbali na kuacha kujihukumu.

Pia kuna hitilafu ya wakati wa kuridhishana, inaweza kutokea mwanamke akawa kamaliza raundi yake ya kwanza, wakati anaingia msisimko wa pili mwanaume anafika kileleni, kinachotokea ni mwanamke kumlazimisha mwanaume arudie tendo kwa muda mfupi tangu amalize, jambo ambalo ni vigumu. Sasa ikitokea mwanaume kachezewa na hana msisimko anapata hofu kuwa haweze, ikijengeka hivyo hata iweje jambo halitawezekana tena. Hivyo ni bora kupeana muda wa kupumzika kabla ya hatua ya pili ya mchezo.

Pale inapotokea hamasa ya kurudia haipo fikra za mwanaume zisipewe nafasi ya kushindwa kwani nyakati, mchoko, makujukumu, hofu za maisha na mambo kama hayo yanapokuja katika siku ya kustarehe ni wazi kuwa kiwango cha ufanyaji mapenzi kitakuwa chini na hali hii huwatokea wanaume wote, hata walio hodari wa kwenda raundi kumi kwa siku.
Sambamba na hilo wanawake wanashauriwa kutoonesha kujali pindi inapotokea hali hiyo, badala yake wawaambie wenzao kuwa siku hiyo inatosha hata kama hawajatosheka, lengo ni kuondoa hofu ambayo ndiyo msingi wa wanaume kuishiwa uwezo wa kufanya mapenzi. Hata hivyo maudhi, kufanya mapenzi na usiyempenda, msongo wa mawazo na kutokuaminiana huchangia kupoteza msisimko wa kuwa ‘kidume’.

Ushauri wangu ni kwamba chochote ambacho unataka mwili wako ukifanye lazima uuzoeze. Ukizoea kuamka saa 12 asubuhi mwili utatii kanuni hiyo. Na ukizoea kufanya mapenzi kila siku mara mbili au tatu hali itakuwa hivyo. Mwisho katika sura hii ni vema wanaume na wanawake wakajifahamu kuwa uwezo wa kufanya mapezni unapungua kufuatana na umri isitokee mtu akakosa raha kisa hawezi kwenda mara nyingi kama zamani wakati anajua kabisa umri wake umekuwa mkubwa.
Jamani kutafuta nguvu za ujana zirudie uzeeni ni kujipa taabu ya bure. Firbath Bayi hawezi kutimua mbio kama alivyokuwa zamani! Ukiona umeingia kwenye utu uzima na mwili wako unaishiwa uwezo, kubaliana na hali. Lakini jambo la kushangaza siku hizi hata vikongwe wanapanga foleni kwa waganga kutafuta tiba ya kufanya mapenzi mara tatu kwa siku! Mapenzi yanataka uwezo wa akili na mwili tusishindane na uwezo asili tutapoteza muda na pesa bure.

Tatizo la mwisho ambalo nalo linatajwa kuwasumbua zaidi wanaume ni maumbile madogo ya uume. Wanaume wengi wamekuwa wakilalamika kuwa maumbile yao yanawazuia kuwapa dozi wapenzi wao. Lakini kama nilivyosema huko nyuma kwamba mapenzi hayana kanuni kwamba lazima mtu awe hivi ili amtosheleze mwenzake. Kinacholeta raha katika mapenzi ni hisia, hii ikiwa na maana kwamba mwanaume au mwanamke anaweza kufurahia mapenzi kwa kutomasana na kuhamasishana kwa viungo vingine vya mwili na kujikuta wameridhika hata bila ya kuingiliana.

Kwa maana hiyo wale ambao wanamaumbile madogo wanaweza kutafuta wanawake ambao nao wanamaumbile ya aina yao. Baadhi ya watalaam wanasema kwamba kwa kawaida umbile la nyeti za mtu linakwenda sambamba na urefu wa mwili wake. Kwa maana hiyo wanawake wafupi, ingawa si wote wanatajwa kuwa na nyeti zenye ukomo mfupi zaidi ya warefu na wembamba wa umbo.
Mbali na chaguo la mtu mwenye kuendena naye umbo, wanaume wenye kasoro hii wanatakiwa kujifunza sana michezo ya kimapenzi ambayo itawasaidia kuwafikisha kileleni wapenzi wao. Ni muhimu kwao kutumia sanaa na mitindo inayopunguza umbali na ukomo wa nyeti za kike.
Mwisho ni misingi ya tiba hii:

MOJA ni kuepuka hofu. Ikitokea siku moja umeshindwa katika tendo haina maana una kasoro, bali ni hali ya kawaida, hivyo usiingize huzuni na hofu utakuza tatizo. Hivyo kwa wale wenye tatizo hili wapunguze wasiwasi na wajiamini kuwa hawana tatizo. PILI, nguvu za kiume zinahitaji mwili wenye nguvu, hivyo ni busara kula lishe bora na kufanya mazoezi yasiyokuwa makali sana. TATU, kumfundisha mwanamke namna ya kukusisimua. NNE, kuepuka mawazo ya kuhuzunisha wakati wa tendo. TANO, kupata muda wa kupumzisha mwili. SITA, kuepukana na pupa, tumia muda usiopungua dakika 20 kufanya romance. SABA, kujiamini KISAIKOLOJIA

Saturday, February 5, 2011

FFU WAWAKUNGÚTA WAFANYAKAZI WA GLOBAL PUBLISHER

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publisher jana walijikuta wako katika kizaizai baaa ya askari wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU kumpiga mfanyakazi mwezao wakidai ni mmoja wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar-es-Salaam waliokuwa wakiandamana. Lakini hata hivyo baadae waligundua taarifa zao za kiitelejinsia hazikuwa sahii. Picha zote kwa hisani ya Global Publisher

Askari wa FFU wakimsaka mfanyakazi huyo karibu na Ofisi

Askari hao wakielezwa kuwa wanomtafuta hakuwa katika maandamano

FFU wakitumia mabavu kumtoa mfanyakazi huyo

Mfanyakazi akiomba msaada kwa wafanyakazi wenzake

FFU wakimpa kipigo kikali mfanyakazi huyo.


Wafanyakazi wakimnasua mwenzao kutoka katika kipigo kikali cha FFU

Mfanyakazi huyo akiwa ahamini kama amenusurika

Wazee wa Kiintelejensia wakiondoka kwa aibu bila mafanikio









Friday, February 4, 2011

UDSM WATAKA KUANDAMANA LEO



Wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam maarufu kama Mlimani walipanga kuandamana leo kuanzia chuoni hadi Ikulu wakidai nyogeza ya fedha ya chakula.

Lakini hadi kufikia saa mbili asubuhi walikuwa bado hawajapata kibali cha maandamano hayo. Askali wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU waliolionekana wakiranda mitaani tayari kwa kutuliza maandamano hayo.

HALI YA UTULIVU MISRI YAZIDI KUWA TATA

Hali ya usalama na utulivu katika Nchi ya Misri imezidi kuwa tata kutokana na Mapigano kati ya Waandamanaji na wale wanaomuunga mkono rais Hosni Mubarak.



Thursday, February 3, 2011

AY AANGUSHA MZIGO MPYA NA TRINITY

Mwanamziki wa Bongo Fleva AY ametoa wimbo mpya na Miss Trinity, mdada mwenye makazi yake huko California nchini Marekani. 

          
Wimbo huu ambao unaoitwa Good Look umepikwa na Hermy B una historia ya Afrika Mashariki kiaina. Wakati audio imepikwa jijini Dar-es-salaam,video imefanyiwa makeke jijini Kampala nchini Uganda. Hapa tunakupa fursa ya kusikiliza kwanza wimbo katika audio, kisha  hapo chini ni video ya Good Look.

Wednesday, February 2, 2011

MAANDAMANO YA KUMPINGA RAIS WA MISRI YAENDELEA

Maandamano ya wananchi wa Misri  kupinga serikali iliyo chini ya rais Hosni Mubarak yamezidi kuendelea huku wakishinikiza rais huyo kujiuzuru.

               Mtoto akiwa na picha inayomkashifu rais wa Misri
Raia wakiswali kwa pamoja na wanajeshi wa nchi hiyo
 
 


Mama wa Ki-Misri akiwa na bango kubwa.
Mzee akiwasalimia wanajeshi baada ya kuamka asubuhi.


Wakisali mbele ya vifaru vya jeshi huko Misri.

Kijana akilalamika kwa uchungu.