Advert

java

Thursday, December 15, 2011

Matokeo ya Darasa la saba.....

WALIOFAULU WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 90.1

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bw. Philipo Mulugo, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam jana, kuhusu matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba, Mwaka 2011. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw.Selestine Gesimba. (Majira)

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limefuta matokeo ya watahiniwa 9,736 waliofanya mtihani wa kumaliza.
darasa la saba mwaka huu baada ya kubainika kufanya udanganyifu. Pia wanafunzi 567,567 kati ya 983,545 waliofanya mtihani huo ambapo wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90.1 wamechaguliwakuingia kidato cha kwanza katika shule za sekondari za Serikali. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bw.Philipo Mulugo, alisema.

Alisema kati ya wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu wapo wavulana 4,943 na wasichana 4,793. Alitaja aina za udangayifu waliofanya kuwa ni pamoja na watahiniwa 94 kukutwa na karatasi na rula zenye majibu pamoja na viatu aina ya ‘yeboyebo’, zikiwa na majibu ya mtihani. Alisema wanafunzi hao walikamatwa katika Halmashauri za Bukoba mkoani Kagera, Muheza mkoani Tanga, Maswa mkoani Shinyanga, Sumbawanga mkoani Rukwa, Mtwara, Lindi na Tarime mkoani Mara.

Akizungumzia malalamiko ya kuwepo kwa wanafunzi wanaofaulu mtihani huo bila kujua kusoma na kuandika, Bw.Mulugo alisema wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, watafanya mtihani wa kujipima kabla ya kuanza masomo. “Mwanafunzi ambaye itabainika amejiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi husika, Mwalimu Mkuu wa shule aliyotokea mwanafunzi na msimamizi wa mtihani watachukuliwa hatua za kinidhamu," alisema.

No comments:

Post a Comment